Ile Sherehe ya Muungano na Utamaduni wa Tanzania ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu sana na watu wengi, jana ilifunika vibaya sana ambapo mamia ya watanzania, wageni toka nchi mbalimbali na NGOs za kitaliano zifanyazo kazi Tanzania kuudhulia kikamilifu.Sherehe hii ilifanyika kwenye ubalozi wa Tanzania mjini Roma kuanzia saa kumi jioni.
Mgeni rasmi alikuwa ni kaimu balozi Mh. Salvatory Mbilinyi ambaye alitoa speech nzuri sana juu ya muungano kati ya Tanzania bara na visiwani na umuhimu wa Watanzania kwa pamoja kudumisha utamaduni wetu. Maonyesho ya mavazi ndio yalifunika kwa sana na pia chakula cha kitanzania kilifurahiwa na wengi.
Kwa niaba ya mwenyekiti wa jumuiya na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome kwa ujumla napenda kuwashukuru sana wale wote waliotusaidia kufanikisha sherehe hii kwa namna moja au nyingine. Shukrani za dhati ziende kwa ubalozi wetu kwa msaada wa hali na mali waliotupatia. Mungu Ibariki Africa Mungu Ibariki Tanzania.
Katibu wa Jumuiya,
Andrew Chole Mhella
Mh. Kaimu Balozi Mh. Salvatory Mbilinyi akielezea umuhimu wa muungano na kudumisha utamaduni wa Tanzania.
WAKATI WA MAONYESHO MBALIMBALI YA MAVAZI YA KITANZANIA.
Kwa habari kamili na mapicha kibao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...