Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana (kushoto), akimpa mkono wa pongezi Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi Doris Malulu, baada ya kupokea juzi jengo la wodi ya kinamama la Hospitali ya Mwananyamala lililofanyiwa ukarabati kwa msaada wa TBL. Wengine kulia ni Mhandisi wa TBL, Bw. John Malisa,
Meneja Miradi Maalumu wa Kampuni hiyo, Bi.Emma Oriyo na Muuguzi wa Hospitali hiyo, Baraka Kapinga
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana akizungumza na maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), baada ya kupokea jengo la wodi ya kinamama katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam lililokarabatiwa kwa msaada wa TBL. Kutoka kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Bi. Doris Malulu, Meneja Miradi Maalumu wa TBL, Bi. Emma Oriyo, Muuguzi wa hospitali hiyo, Bi. Baraka Kapinga na Mhandisi John Malisa wa Kampuni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana (wa pili kulia), akitoka kukagua choo cha wodi ya kinamama katika Hospitali ya Mwananyamala kilichofanyiwa ukarabati mkubwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL Bi. Doris Malulu, Meneja Miradi Maalumu wa TBL, Bi. Emma Oriyo na Mhandisi wa wa kampuni hiyo, Bw. John Malisa.Hafla hiyo ya kukabidhi choo na jengo la akinamama ilifanyika hospitalini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana (mbele), akisindikizwa na Mhandisi wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. John Malisa (kulia) kukagua choo cha wodi ya kinamama ya Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, kilichokarabatiwa na TBL.Kushoto ni Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo.
hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2011

    HAYO NDO MANENO TUYOTAKA KUSIKIA!!! WALEWESHENI, WAZICHAPE, WAUMIZANE HALAFU WAENDE HOSPITALI KUTIBIWA. WELL DONE WANA KILEVI

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2011

    mhhhhhhhhh kina nanii kaeni mkao wa kula

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...