Mjumbe wa kamati ya miundombinu ya Bunge na Mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Mh. Mnyaa Mohamed Habib, akifafanua jambo kuhusiana na mambo ya mawasiliano wakati walipotembelea makao Makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania yaliyopo mlimani city jijini Dares Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Dietlof Mare akiongea na wajumbe wa kamati ya miundombinu ya Bunge kuhusiana na uendeshaji wa kampuni yake wakati kamati hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo kwa lengo la kuangalia uendeshaji wa mawasiliano katika kampuni hiyo.
Mwenyekiti wa kamati way a miundombinu ya Bunge na mbunge wa Kigoma mjini Mh. Peter Serukamba katikati akiongozana na Mkurugenzi wa kitengo cha sheria wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Godwin Ngwilimi(kushoto)wakati kamati ya miundombinu ya Bunge walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo kujuonea namna wanavyoendesha shughuli zao,kulia Meneja wa mambo ya nje na yakiserikali wa Vodacom Tanzania Bi. Nector Foya.
Mkuu wa kitengo cha uwangalizi wa Mitambo ya Vodacom Tanzania Bw. Erasto Haule akiwaelezea wana kamati ya miundombinu ya bunge jinsi wanavyoendesha mitambo 1200 Tanzania nzima mara walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo mlimani city jijini Dares Salaam.
Mjumbe wa kamati ya miundombinu ya Bunge na mbunge wa Lushoto Mh. Henry Daffa Shekifu akimuuliza swali Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Najenjwa Mbagga(mwenye nyekundu)kuhusiana na huduma za kitengo hicho cha wateja wakati kamati ya miundombinu ya Bunge walipotembelea makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...