Hayawi hayawi yamekuwa wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumeremeta katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar ni wadau  Julius Nalitolela na  Bernedetha Alex wakiwa katika pozi la picha.

 Bwana harusi  na bibi harusi  Julius Nalitolela na Bernedetha Alex wakigongesheana gra shampeni katika mnuso wa harusi yao hiyo
 Bwana harusi Julius Nalitolela akisaidiwa na babu yake Patrick kupita juu ya migongo ya  wazazi wake wakati alipokuwa akiingia ukumbini Royal Skyline  ikiwa ni sehemu ya kudumisha mira ya Wayao wa Nandenga Masasi Mtwara ,baada ya kufunga ndoa katika kanisa la St,Albano jijini Dar es Salaam.
Bibi harusi Benedetha Alex ambaye kabila lake ni msukuma akielekezwa mila na desturi za wayao na babu wa mme wake Julius Nalitolela mzee Patrick wakati alipokuwa akiingia ukumbini kwa kupita juu ya migongo ya akina mama wa Kabila la Wayao wa Masasi Mtwara. katika harusi iiliyofungwa katika kanisa la St.Albano na kufuatiwa sherehe kubwa illiyofanyika ukumbi wa Royal Sklin jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2011

    Eeh jamaa eeh kweli kuna mila na mila:-) Sasa yote haya ya nini toba:-)? Ukija ukitengua mguu au uka-slip juu ya mgongo wa mtu? Sielewi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2011

    hizi ni mila za kweli? poleni sana hao mlio pitiwa migongoni. hawa watu kama walikua wanafuata sana mila wange wavalisha maharusi kaniki au majani. bibi harusi be careful kwasababu this is just the beginning. mila za hao watu ni nyingi sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2011

    sasa mbona bibi harusi yeye hakuvua viatu siakuwa anawaumiza wenzie na viatu ukizingatia viatu vinavisigino mila zingine ni hatari kuliko malaria

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2011

    nw this is jst painful...the significance of this is very vague..anyway..hongereni mwaya!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2011

    Shemeji Peter Nalitolela wa Mologolo ze Mzumbez yuko wapiiii?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2011

    Kaaazi kweli kweli ! duh !!! nimeweka mkono shavuni !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...