MaishaMema Education & Training Centre ni kituo cha Elimu, Mafunzo, Utafiti na Ukuzaji Maarifa...Kituo kinatangaza semina ya siku moja kuhusu MBINU ZA UANDISHI BORA WA VITABU... Semina imelenga katika kuwajengea washiriki uwezo wa kufanya kazi na kituo katika mradi wa SEXUALITY EDUCATION AND AWARENESS PROJECT CAMPAIGN ( SEA Project ), mradi unao ratibiwa na kusimamiwa na kituo na ambao umelenga katika kutoa elimu ya ujinsia, afya, uzazi wa mpango, haki,wajibu na kujitambua kwa wanawake kwa njia ya vitabu.

SIFA ZA WASHIRIKI
Awe mwanamke mwenye sifa zifuatazo:
1. Umri miaka 18 hadi 40.
2.Elimu kidato cha nne, sita na kuendelea.
3.Mchapakazi na anayejituma na awe mwenye 
wito wa kweli wa kazi ya uandishi vitabu.

LINI: Jumamosi, tarehe 04/06/2011

MUDA : Saa nne kamili asubuhi.

WAPI: PERFECT VISION SECONDARY SCHOOL.

IDADI YA WASHIRIKI WANAO HITAJIKA: Thelathini na Tisa Tu. ( 39 )

FAIDA ZA KUSHIRIKI KATIKA SEMINA HII: Washiriki wote thelathini na tisa watapata nafasi ya kuungana na wenzao kumi na moja ambao tayari wameshapatiwa mafunzo katika kufanya kazi ya uandishi wa vitabu katika mradi huu, ambao unaanza rasmi tarehe 01 June 2011 kwa washiriki kumi na moja ambao tayari walishapatiwa mafunzo

Fomu za kujiandikisha katika semina hii zinapatikana  katika ofisi zetu zilizopo katika shule ya sekondari PERFECT VISION iliyopo nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA...

Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 03/06/2011.... ..

WAHI FOMU YAKO MAPEMA, KWANI IDADI YA WATU WANAO HITAJIKA IKIKAMILIKA, TUTASITISHA KUTOA FOMU.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA: 
0652458398 AU 0788363058..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...