Mh. Mizengo Pinda
Kaka Issa Michuzi,

Pole na majukumu makubwa uliyonayo ya kuihabarisha jamii.
Tunakuomba utuwekee barua yetu hii ya wazi kwa mheshimiwa Waziri Mkuu katika blog yako. Tunashukuru sana kwa moyo wako wa kusaidia wengine.

Asante sana.
WANAFUNZI WA KITANZANIA 
CHUO KIKUU CHA URAFIKI LUMUMBA, MOSCOW-URUSI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2011

    Tumechoka sasa,na mwaka huu lazima tudai haki yetu kwa maandamano maana ndivyo serikali inavyotaka,yaliyotokea mwaka 2008 mwaka huu lazima yatokee kama kurudishwa nyumbani na waturudishe!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2011

    Ni aibu sana kwa serikali yetu,kwa nini inawapeleka watoto mbali sana kisha wanashindwa kuwahudumia.Hii yote inatokana na ufisadi uliokithiri ndani ya serikali yetu.Matokeo yake watoto wanafanya mambo ambayo hayastahili ili wapate pesa za kujikimu.Kwa mfano nina nilipata kusikia habari za ushoga kwa baadhi ya wanafunzi wa kitanzania waliyopo urusi.Sasa hii ni hatari sana.Namuomba waziri mkuu kwa uungwana wako wasaidie hawa vijana.Mdau Manzese Darajani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2011

    SUBIRINI JAWABU LA PINDA ATAKALOWAPA ATAWAMBIA "NIMESIKIA" KAMA ALIVYOULIZWA BUNGENI KHS WAZIRI KUISHI HOTELI............ATI MTT WA MKULIMA........

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2011

    Inasikitisha sana kuona kuwa serikali yetu haitaki kabisa kusikia vilio vya wanafunzi, hasa wa vyuo vikuu. Lakini inasahau pia kuwa hao ndiyo viongozi wa kesho wa taifa hili. Wapeni haki zao ili tupate wasomi bora na siyo bora wasomi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2011

    nipishe mimi nimalize maaama hili ni janga sasa

    ReplyDelete
  6. Poleni ndugu zangu !!!! ni wazi inajulikana pesa zenu zinatiwa kapuni na mijitu wizarani

    La msingi.....

    Anzisheni mtiti kama wenzenu walio uanzisha mwaka juzi maana inaelekea mpaka pachimbike ndo wadau washtuke kuwa mnaumizwa....ila kumbukeni kufungasha document zenu za muhimu nakuziweka kibindoni ready to be sent back home via DHL maana likinuka mtafungashwa ka sijui nini aiiseee..... {chonde usikae na vyeti vyako au kurudi navyo mwenyewe maana ma mafia watakunyanganya Airport Tz}

    kila la kheri,ila msiingie kwenye biashara za kujidhalilisha e.g: Ugasho na dada zetu kuwa jamvi la wageni....

    nihayo tu kwa leo...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 20, 2011

    Kuna wakati nahisi kama akili yangu inataka kusimama vile [yaani kutofanya kazi kabisa] na hasa ninaposoma habari kama hizi.

    Napata shida na akili kutaka kusimama kutofanya kazi kwa sababu ukienda leo pale Bodi ya Mikopo au huko Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, utapewa mashairi mazuri sana [MANENO YENYE SABABU 7 X 70] ya kwa nini hawa wa Bodi ya Mikopo wanafanya hivi.

    Niliwahi kuhoji uhalali wa kuwepo Bodi ya Mikopo na nikasema hebu TUIBINAFSISHE ili tumpe 'KABURU' mmoja aihudumie kwa miaka 3 kisha tuone kama kuna sababu za namna hii zinaweza kutokea.

    Mimi nasema Watanzania hawana tabuu jamani hata kama RAIS wao angekuwa Kobe au hata Rais wao angekuwa Mtoto sisi hatuna taabu, tatizo lipo juu. Huko kwa waheshimiwa.

    Ningekuwa na Mamlaka kamili siku moja ningeamka asubuhi na kuwapa barua za kuwapumzisha watumishi wote wa Bodi ya Mikopo na kingefuatiwa kuachishwa kazi na wanaingie wengine wapya. Nadhani hili lingekuwa fundisho.

    Sasa wewe subiri uone MASHAIRI [Majibu] kutoka hiyo Bodi ya Mikopo ba huko Wizara ya Elimu ambapo unadhani kuna kazi wanafanya kazi kuiba fedha za watu na kuwapa Watawala.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 20, 2011

    MICHUZI NAOMBA UICHAPISHE HII KWANI SITUKANI NI MAWAZO YANGU TU.....JAMANI SERIKALI MUWE MAKINI SANA NA HAYA MAMBO,NAJUA KABISA MLIFANYA TATHIMINI MKAONA MNAWEZA KUWASOMESHA HAWA WANAFUNZI,HAMJAKURUPUKA TU NA KUWAPELEKA, MMEWAPELEKA HALI MKIJUA KABISA KWAMBA MNAWEZA KUWASOMESHA KWANINI MNAWATESA LEO???SUBIRI NIWAAMBIE KITU HAWA NDIO VIONGOZI WA KESHO AMBAO MNATEGEMEA KUWALETEA MAENDELEO AMBAYO NYINYI MMESHINDWA KUYALETA...KUWENI MAKINI HAWA MKIWACHEZEA NDIO WATAKUWA WA KWANZA KUSHIKA BUNDUKI KUWACHINJA,SIOMBI JAMBO HILI KUTOKEA KWANI WOTE TUTAPATA TABU,KAMA KUNA UWEZO WA KULIEPUKA KWANINI MSILIEPUKE?NAAMINI KABISA KWAMBA MLIKUWA MNAJUA KUNA WATOTO RUSIA NA MLIJUA MNA HELA KAMA MNGEKUWA HAMNA MSINGE WAPELEKA....MAMBO KAMA HAYA NI HATARI SANA KWA TAIFA,KAMA KUNA MTU ANAIBA HELA ZA HAWA WATOTO BASI ASHUGHULIKIWE HARAKA!!NI HAYO TU..VIONGOZI KUWENI MAKINI WATU WAMECHOKA SANA SASA.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 21, 2011

    I fail to understand anayepewa hela atume ni nani?maana kuna wanafunzi wengine wanamaliza this year nimeskia kuwa hawatopewa vyeti koz ada haijalipwa au imelipwa nusi,so mnataka warudi home bila cheti?na wameshakaa huku miaka sita sijui saba!kah ni aibu kwakweli,hadi warusi wanashangaa mnooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...