Bhoke
Bhoke, mwakilishi wa Tanzania katika Big Brother Amplified 2011 amerejea nchini jana usiku na leo ataongea na wanahabari saa tano asubuhi hii katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar es salaam, kwa mujibu wa afisa uhusiano wa MultiChoice nchini, Barbra Kambogi

. Kuondoka katika mchezo wa Big Brother ambao mshindi anaondoka na kitita cha dola laki 2 za Kimarekani kumehitimisha ushiriki wa Tanzania katika mchezo huo kwa  mwaka huu ambao unaoneshwa hai katika channel ya Mnet kwa masaa ishirini na nne siku zote saba za wiki. 

Mshiriki mwingine, Lotus, alienguliwa katika mchuano huo majuma mawili yalopita kufuatia sakata la kumzaba kibao mshiriki mwenzie kinyume na taratibu. Bhoke ameenguliwa kutoka  katika jumba la Big Brother sambamba na mshiriki  Ernest toka Uganda ambao kwa pamoja wameonekana wakiwa wapenzi na wakifanya mapenzi  mbele ya kadamnasi siku moja  kabla ya kuaga wenzao waliosalia.

 Video ya uhusiano huo wa mapenzi na mshiriki wa Uganda zimesambaa katika mitandao kadhaa (sio Globu ya Jamii) na kuzua maswali kibao endapo kama maadili ya Kiafrika yanazingatiwa katika jumba hilo. Akijibu swali baada ya kuenguliwa Bhole alisema kwamba kilichoonekana katika jumba hilo hakikuwa maigizo bali ni kweli 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2011

    Mchafu sana huyo dada. Alienda big brother kufanya ufuska hadharani na Ernest wa Uganda. Serikali itabidi iliangalie sana hili maana ni kama tunaenda kuonyesha jinsi gani tunafanya ukahaba na umalaya. Hata vita dhidi ya UKIMWI inaonekana ni kazi bure!! Taifa limeaibika sana na amewaaibisha sana akina mama wa Tanzania. Hata hao wanahabari anataka awaambie nini? Kila leo vituko, fujo na umalaya. Michuzi, muulizeni huyo dada kwa nini ameliambisha taifa hivyo??
    Mdau niliyeumizwa na picha ya ngono ya Bhoke iliyoonyeshwa kwenye michuzi Juniour

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2011

    Yaani Bhoke hicho kitendo ulichokifanya na Ernest chini ya blanketi hakikuwa kizuri. Anyway ushauri wangu kwa Multichoice Tanzania ni kuchagua washiriki wazuri ambao wapo fun, wasiangalie kuwa mtu anaongea kingereza vizuri ikawa ndio kigezo pekee. Huyo Bhoke kutwa alikuwa ana lala na hata kuongea kwake ilikuwa kwa nadra sana. Lotus alikuwa muwakilishi mzuri ila tu hasira zilimzidi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2011

    ningekuwa na uwezo, aki ya nani. Marukufu kwa Mtanzania kushiriki BBA.... Bado sijaona BBA ina malengo gani chanya kwa washiriki wake, zaidi ya kuwaweka watu kwa pamoja siku 90 na kuwajengea moyo wa kufanya UFUSKA..Hizo task zenyewe wanazofanya zitawasaidia nini ktk ulimwengu huu wa sasa. Huwa najiuliza hivi mtu unaweza kuacha kazi yako, familia yako n.k ukaenda kushindania zawadi moja (inayomendewa na watu lukuki) then hata ukiwa wa pili umeshindwa huna kitu zaidi ya U - Famous uchwara.... (Jamani watanzania (kaka kwa wadada) tufunguke. Kweli binadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2011

    AMETUDHALILISHA SANA HUYU DADA........SIJUI HAO WAZAZI WAKE WANAJISIKIAJE KAMA MIMI MBONGO WA KAWAIDA IMENIBOA KIASI HIKI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2011

    NAFEEL KIZUNGUZUNGU.

    LOTUS ALIRUSHA NGUMI AKATOLEWA TUKASEMA NI ZUMBUKUKU....HUYU BHOKE KAGAWA URODA HADHARANI!

    KAZI IPO! LABDA WATU WARUHUSIWE KWENDA NA WAKE/WAUME ZAO VINGENVO WATATULETA NGOMA HAWA WATU.

    ENEWEI TUSUBIRI TUMSIKIE ATAONGEA NN.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2011

    Waandishi wamuulize hili swali.

    http://www.gistexpress.com/2011/06/07/video-m-net%E2%80%99s-big-brother-amplified-series-more-like-a-porno-house/

    Ametuaibisha sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2011

    huyu Nae ndio nini sasa? karudi na shemeji?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2011

    Pole yakee, alizani kujidhalilisha kutampa umaarufu! Shame on her! Hakututendea haki watanzania maana kimsingi alipokuwa pale aliwakilisha watanzania, shame on her again!! Anatabia chafu ambazo zinakera, hafai hafai hafai!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2011

    michuzi weka comment yangu bana , mbona mnaibania lakini.... hali hewa haijachafuliwa hilo liko wazi

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2011

    Huyu ameonesha nusu ya utamaduni unaojengeka Tanzania hivi sasa, ilipoanza Big Brother nafikiri 2004 nilikuwa uingereza, aliyeshinda lile shindano alikuwa ni gay, mwanaume lakini mule ndani aliishi kama mwanamke na alikuwa anajiremba, mspanish. Lakini hajapata kufanya ngono na hawakupata kumwona jinsia yake. Hivyo kwamba ukiingia Big brother lazima ufanye ngono mimi sielewi kabisa. Waafrika tunapenda kuinga mambo lakini utamaduni wa kiafrika ni mzuri. Pale ndio pahala pa kuonesha tamaduni mbali za afrika na sehemu za utalii. Yesu bora aje, tuondoke nae tuliookoka, tuwaache na dunia yenu. Bhoke na wazee wako nendeni kanisani mkatubie. Sio sifa ya mwanamke hiyo. Yule aliemnasa kibao mwanamme ndio mtoto wa watu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2011

    dada hujaiabisha tanzania bali umejiabisha mwenyewe na wazazi wako kwani hata kama uliiwakilisha Tanzania ila tanzania haijakutuma ukafanye ufuskaa ila tabia yako chafuu na ulimbukeni wako wa maisha ukaona uigee ili uonekane mbora katika washiriki kumbe masikini umejitia jiti la roho.. masikini dada yangu si bora ungeenda kanisani kushindania kuabudu mungu maana saivi huna umaarufu wala hujapata ushindi ila umepata aibu pole ila usisahau kupima ukimwiiii maaana isije kuwa marehemu mtarajiwa
    by mimi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2011

    INFACT BHOKE IS SUCH A BORE AND WANTED TO GET FAME BY FORCE,WHY DID YOU COME TO THE SHOW WHEN YOU HAVE NOTHING TO OFFER?
    YOU SHOULD FEEL ASHAME OF YOURSELF FOR TELLING BIG BROTHER YOU DON'T REGREAT ANYTHING IN YOUR LAST NOMINATION CHAT SESSION.
    Ni mimi mdau mwenye hasira kali na huyu binti I WISH LOTUS WOULD BE STILL IN THE GAME AND SLAP BHOKE FOR ME no offence I am just saying LOL

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2011

    Wooooooooooooooooooooooote manaonea tu mbona nyie hamuendi bi brother mwenyewe kasema kuwini dola laki mbili it's not a lelemama. Mumuache Bhoke wa watu uroda katoa yeye aibu kapata yeye na familia yake. Amegawa uroda na amerudi angepata ushindi mnesema kama alitoa uroda.......???????????

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 09, 2011

    STUPID WOMAN,INAFAA HATA HUKO ANAKOFANYA KAZI YA KUTANGAZA AFUKUZWE MAANA AMELETA AIBU,NI HII BBA INAFAA IPIGWE MARUFUKU AU IKIBIDI WATANZANIA WASIRUHUSIWE KUSHIRIKI,PIA NJAA YETU ITATUFIKISHA PABAYA,ETI AMETUWAKILISHA VIZURI ???KI VIPI ??KWA UFUSKA ??JE KWA SAILI HII TUTAWEA KUMALIZA UKIMWI ??hALAFU UNAKUTA ANAPOKELEW UWANJA WA NDEGE NA WAZAZI,KWELI TANZANIA BADI KAZI IPO,NA NJAA IMEZIDI PIA WATU BADO TUPO VERY IGNORANT,SHAME ON YOU STUPID BHOKE !!!NJAA ITAKUUA NA UKIMWI.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 10, 2011

    UWiiiiiiiiiiiiiiiiiii, Mimi huyu dada kwa kweli sitaki hata kumwona kwa kitendo cha kimbwa alichokifanya jamani. Natamani kulia kwa sababu ni aibu kubwa mno ametutia si Watanzania na hasa wanawake na zaidi sana wazazi wake. Haiwezekani mtu uwe mjinga kiasi kile wakati fika unajua kule kamera 24 hrs ziko on. Yaani ningekuwa mimi mzazi wake marufuku kuniita mzazi wala nyumbani kwangu asikanyage. Lile ni tendo la siri kwa ajili ya siri ili siri iwepo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...