Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein |
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Katibu Mkuu, Wizara ya Ustawi wa Jamii, na Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Bi Fatma Gharib Bilal hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Hafla ya kuapishwa kwa Katibu Mkuu huyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Seif Sharif Hamad, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Waziri wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, na Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar.
Viongozi wengine waliohudhuria kuapishwa kwa Katibu Mkuu huyo ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo Duniani, UNDP Bwana Soro Karna pamoja na wawakilishi wa UN na mashirika yake ya UNFPA, WHO wanaofanya kazi zao hapa nchini na viongozi wengine wa serikali.
Fatma Bilal kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amewahi kufanya kazi katika sehemu mbali mbali hapa nchini zikiwemo Wizara ya fedha na ualimu ambapo kabla ya uteuzi wake alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watu Duniani UNFPA.
Katibu Mkuu huyo, anachukua nafasi hiyo baada ya kuachwa wazi kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, na Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto, Bi Rahma Mohd Mshangama.Bi Fatma Gharib Bilal ana shahada ya pili ya uchumi.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
20/06/2011
Ni mawazo yangu tu kuwa press release kama hizi za kuteuliwa viongozi fulani zitolewe na picha (pasipoti) ya huyo mteuliwa na sio picha ya aliyemteua. Kwa maana huyo aliyeteuliwa watu wengi hawamjui na anayeteua -raisi wote twamjua.
ReplyDeletePili hizi official photo za maraisi wetu, kiwango chake kingekuwa cha juu zaidi iwapo zingeonyesha bendera ya taifa kwenye background na pia raisi awe amechomeka ki medani kidogo cha bendera ya taifa kwenye kola ya suti kushoto? Angalia official photo ya Obama www.http://change.gov/newsroom/entry/new_official_portrait_released/
Hii inaleta maana zaidi kwa picha hizo, maana zinakuwa si picha ya mtu-raisi tu, bali picha hizo pia zinaitangaza nchi yetu kwa watu hata wasiomfahamu ua wasioifahamu nchi yetu.
Alex bura, dar