Mh. Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Dar es salaam kufuatia agizo la pili la Hakimu wa Mahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani katika kesi inayomkabili ya kufanya kusanyiko lisilo halali mkoani Arusha tarehe 5 Januari 2011.


Akitoa hukumu dhidi ya washtakiwa wengine waliojisalimisha mahakamani baada ya kushindwa kuhudhuria katika mahakamani hapo Mei 27, 2011, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alisema kitendo cha mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo kushindwa kujisalimisha labda anataka kukamatwa na Polisi.
Picture
Mahakama hiyo awali iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Bw. Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini), Bi. Josephine Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba.


Pamoja na washtakiwa na wadhamini wao kutofika mahakamani, hata Mawakili wao, Bw. Method Kimomogolo na Bw. Albert Msando pia hawakuwepo mahakamani wakati hati hiyo inatolewa, lakini washtakiwa Bw. Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Bw. Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwakamatwe kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.


Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Nai Steven, Mathias Valerian, John Materu, Daniel Titus, Juma Samuel, Walter Mushi, Peter Marua na Erick Makona.

Hakimu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamataa au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo wala mdhamini wake, hivyo Ofisa Inchaji wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama ni si vinginevyo, “Wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo wanapatikana na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu. Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa Inchaji amkamate na kufikishwa mahakamani.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2011

    kaka haupo juu ya sheria mahakama ni muhimili unaojitegemea usifikiri upo juu yake bunge ni muhimili wa tatu baada ya serikali ni mahakama alafu bunge sheria mnatunga wenyewe mnashindwa kuzitekeleza?msidanganye watu hasa lisu sheria yake kasomea wapi?au UDSM NA CHUO HURIA AU TUMAINI?watakuponza hao ubunge wako haukufanyi uwe juu ya sheria kaka pole sana nguvu ya umma ipo wapi ikutetee?ndio ujue wabongo hawamaanishi
    '

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2011

    CHADEMA wameguuka CUF Zanzibar. Wakipewa uwaziri watatulia!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2011

    Watz bwana we ulieandika wa kwanza mbona unaandika pointless Mbowe amekuammbia yuko juu yasheria? Mbona hata wabunge wa CCM wanavunja sheria hawajawahi kukumatwa? Mi nadhani tusichangie mada isiyotuhusu tufikiria uonevu uliopo na haki zilizopo Tz. Mbona Ditopile aliuwa ila hakufungwa maisha?Mbona rushwa inanuka Tz kila mahali na wala rushwa wanafahamika ila hawasemeshwi. Nadhani kuna something wrong si kwa Mbowe tu. Nadhani tunatafuta kuwa kama Libya na CCM itakuwa imechangia japo hawaoni. Vijana wakifanya biashara wanakamatwa na mgambo wapi waende kama si kuandamana wakitegemea maisha bora?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...