JAJI MKUU  MH. MOHAMED CHANDE OTHMAN (SHOTO) AKIZINDUA KAMPENI HIYO JIJINI DAR ES SALAAM LEO MCHANA
 JAJI MKUU MH. MOHAMED CHANDE OTHMAN CHANDE AKIHUTUBIA WAKATI  AKIZINDUA KAMPENI HIYO JIJINI DAR ES SALAAM LEO MCHANA
WADAU MBALIMBALI WAKIFUATILIA UZINDUZI HUO
 IGP-SAID MWEMA AKITOA HOTUBA YAKE
 
ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISOMA UTENZI
WADAU WALIOSHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA JESHI LA POLIS YA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI
Picha na Habari na Francis Dande 
wa Globu ya Jamii, Dar



JAJI Mkuu Mh. Mohamed Chande Othaman amewataka wananchi kutii sheria bila kushurutishwa kwani kufanya hivyo kutavisaidia vyombo vya utoaji haki kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi zaidi.

Aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo pia  kutaiwezesha  jamii kuishi kwa amani, usalama na utulivu pamoja na kupunguza hali ya watu kuishi kwa mashaka na wasiwasi, kupunguza matumizi ya nguvu na kuimarika kwa mahusiano ya kiutendaji  kati ya vyombo vya dola na wananchi.

"Kwa jumuiko hili ambalo linashirikisha vyombo na wadau wakuu wa utoaji na usimamizi wa haki, ninathubutu  kusema kuwa kampeni hii nimeipokea kwa moyo mmoja na ninaamini kwamba tutashirikiana kwa chachu ya utekelezaji wa mkakati huu kwa vitendo kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria".

Aidha ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali kujumuika pamoja  katika kampeni hii ya kuhamasisha wananchi kutii sheria bila kushurutishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2011

    Uncle, hili suala la kutii sheria ni tatizo kama kansa hapa Tanzania.
    Mifano hai:
    Kwanza: Wakati wa muda wa foleni za magari - utaona si daladala na teksi tu zinaendeshwa pembezoni sehemu za waenda kwa miguu, bali pia magari ya polisi wenyewe, magari ya viongozi wetu, magari ya maofisa kampuni binafsi na hata mabalozi wote mkumbo mmoja, short cut na wanatengeneza foleni zao pembezoni mwa barabara. Waenda kwa miguu, who cares? Huu ni uzunjaji sheria.
    Pili: Kuheshimu taa nyekundu - si daladala wala texi, pia viongozi serikalini, binafsi polisi pia. Wanajeshi ndio wao nadhani nchi nyingine ndio mifano ya nidhamu ya hali ya juu, huku kwetu ndio ovyo kupita taasisi nyingine. Wanadhani nidhamu ni ukiwa kwenye kambi za jeshi tu, kupiga watu, kuruka taa nyekundu, kupita barabara ya mwelekeo mwengine wakati wa foleni ndio kawaida yao
    Tatu: Nchi zeto staarabu hata kwa wenzetu Kenya, Uganda, wana muda wa kufungua na kufunga baa. Wanasheria kuwa kumbi za muziki ziwe ndani (sound proof) na pia sehemu za sharehe zimetengwa. Hapa kwetu nasikia sheria zipo lakini hakuna mfuatiliaji. Madiwani ndio uozo mtupu. Wakazi wa sinza, mwananyamala, temeke, kimara kotekote ni kelele kelele za mabendi na madisko usiku mzima???. Je watoto wanalalaje kwenye nyumba hizo za uswekeni? baa kila baada ya nyumba moja. Sisi Masaki, Msasani, Mikocheni, Ada Estate shwaaari, Sijaona nchi isiyotekeleza sheria kama hii. Ni ajabu watanzania wengi wala hawajuu haki zao za kimsingi kama kuwa na hali ya utulivu bila buguza za kelele (noise polution). Kwa mfano jaribu kwenda Mzalendo pub saa 6 usiku ukitaka kuifunga bendi utakoma - wananchi watakupiga mawe wewe kama mwizi.
    Je shirika kama LAPF linakuwaje kuruhusu jengo lake kutumia wa wapangaji katika shughuli zinazovunja sheria? kuruhusu muziki ya dansi juu gorofani eneo la wazi nilalosababisha sio tu uvunjaji wa sheria bali bughuza kwa wakazi wa Makumbusho, kijitinyama na Mikocheni kwa sauti za bendi usiku hadi alfajiri? Je ndio Corporate Social Responsibility hiyo - kuwatumbuiza na mzika wa open air?
    Nne: Short cut, kutafuta urahisi usiostahili, basi imekuwa tamaduni za watanzania tunaamini kila kitu kinamipango ya kukipata kirahisi isivyostahili. Shuleni hatutaki kusoma tunatafuta feki, Maofisini hatutaki biddii na promotion tunaitaka vilevile tusipoipata lawama
    Tano: Excuses - basi kila liendalo kombo kwenye shughuli yangu basi kuna mchawi wangu anayehusika na sio mimi mwenyewe.
    Sita: Kitu kidogo - karipoti kuibiwa polisi basi umewatengenezea ulaji wao. Inakuwa nani kati ya wewe na mwizi wako ana pochi kubwa
    Nane: Kelele za makampuni ya kutangaza biashara na magari yao, yanapita hata hospitalini na mashuleni wakati vipindi vinaendelea?
    Tisa: Je Kati ya "mchakarikaji mlipa kodi" na "asiyechakarika - halipi kodi bali anakula kodi zenu" Nani Zaidi? Jaza mwenyewe - mimi ni mla kodi, nina V8 na mnaninunulia mafuta shenzi zenu
    Basi mimi nisiyelipa kodi na ninayekula kodi zenu nimeamua kuongeza matumizi yangu mwaka huu, na nimeamua kuwa nyie mnaolipa kodi mtalipa zaidi mwaka huu. Msilalamike basi.
    Jamani wahusika chukueni hatua; Waandishi Habari suala hili ni kubwa laini hamlileti na kulifanjia kampeni
    Take Action Now
    1. Say no to Noise Pollution in our neighbourhood
    (Sema Hapana kwa uchafuzi wa mazingira na bughuza kwa sauti Kubwa za miziki ya densi, kelele za bar, pia ndani ya daladala)
    2. Say no to uncontrolled Bar and Pubs and Clubs
    (sema hapana kwa shughuli za baa zisizodhibitiwa – hapana kwa baa za asubuhi mpaka asubuhi)
    3. Say no to a Bar/Pub established in residential area
    (Sema hapana kwa Bar kuruhusiwa sehemu za makazi ya watu)
    4. Disco & Dance must be performed in sound proof building
    (Disko na mziki wa dansi upigwe ndani ya kumbi zenye kuzuia sauti isitoke nje na kubughuzi jumuiya)
    5. Say no to red traffic light jumpers
    (Sema hapana kwa wanaoruka taa njekundu)
    6. Say no to kitu-kidogo
    (kitu kitogo hapana)
    7. Say no to Madiwani useless – posho tu na porojo za siasa
    (Sema hapana kwa madiwani wasiofanya kazi zao)
    Alex bura, dar

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2011

    hao ni askari kanzu au ni waumini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2011

    sana vijana afande naona mnawajibika kutoa flavour

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2011

    Hii ni sherehe ya Idd-el-Fitr?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2011

    Mdau wa kwanza kutoa maoni....mimi siongezi kitu, yaani ni kama vile umedesa mahali, hivyo vitu ulivyovisema watu wengi vinawakera, hata km wanajua haki zao, waende wapi na kwa nani, maana system ni mbovu...mfano mtu akiwa na vijisenti vyake anaamua kujenga tu bar kwenye makazi ya watu, na hafuati utaratibu...wala hawezi shurutishwa maana ana vijisenti. Sasa tukimbilie kwa nani...mimi nikisema no kwa kila kitu kibaya mwenzangu atasema ndiyo kama ulivyodokeza kuwa "unaweza kujikuta unapigwa hata mawe"...huu ni ushenzi mtupu....Nadhani system yenyewe ibadilike, iweke standards kulingana na sheria...mfano km mtu atajenga ukumbi wa music lazima aweke sound proof, yaani ifuatwe km wanavyofanya kwa Wafamasia (Pharmacists)..kuwa lazima duka liwe na vioo n.k. Jamani Jeshi la Police tusaidieni mitaani tunaumia...wanaovunja sheria wachukuliwe hatua, mbona tunawapeni taarifa na ninyi mnafahamu mambo haya????? Hebu fanyeni kazi yenu sasa, au kuzindua ndo mnasikia raha kuhudhuria?...Mkuu wa jeshi la Police Wapange vijana wako...bado tuna shida mitaani na mabarabarani, na mazingira kwa ujumla...yaani duh, aibu kuyasema haya kila siku jamani....

    ReplyDelete
  6. Naimani kila kitu kinahitaji iniatiative watu katika mahala usika,ikitokea sehemu watu wenyewe hawahitaji ujinga wabar na maclub wanaweza... Tena bila kusubiri sheria za serikali audiwani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...