Uncle Michuzi, Baada ya kusoma kauli mada iliyotolewa na Ndugu Madaraka Nyerere kuhusu ujenzi wa barabara katika mbuga ya kuhifadhia wanyama ya Serengeti nimeona na mie niseme jambo.
Map of Proposed and Existing Roads in the Serengeti Region
Map produced by SavetheSerengeti.org
 Kwanza kabisa nianze kwa kusema nimesikitishwa na mawazo ya Ndugu Madaraka kuhusu katika kufananisha athari ya ujenzi wa barabara na mapito ya wanyama hao katika maeneo yenye wanyama wakali kama samba na mito iliyojaa mamba. Amesahau kuwa kuwepo kwa wanyama wanaokula wanyama wenzao (Predators) ni msawazo maalum katika mizani ya maisha ya wanyama hao. Wenye kula majani wanategemea wanyama wanaowinda katika kuhakikisha kuwa idadi yao inahimili mazingira waliyopo. Na pia Simba na wanyama wawindaji huchunguza kundi kabla ya kuwinda wakiona mwenye matatizo (weak) ndio wanamuwinda hivyo kuacha wenye afya njema wakiendelea.
Athari ya barabara katika mbuga sio tu kwamba itabomoa natural order ya wanyama hao bali itabadili mazingira, je umefikiria suala la uchafuzi wa mazingira utakaotokana na gesi chafu za magari (air pollution) na kemikali zitakazomwagika kama mafuta ya magari, sauti za magari(sound pollution), uchafu utakaotupwa ovyo na wapiti njia, idadi ya wanyama watakakufa kwa kugongwa na magari, njia rahisi kwa majangili kuuwa wanyama hao, idadi ya askari pori watakaohitajika kulinda wezi wa nyara, uharibifu wa mioto asilia na kujenga mipaka isiyo asilia.  Hayo ni kwa upande wetu na jinsi gani wanyama watakavyopokea kuwepo kwa barabara na mambo yatakayoletwa na hiyo barabara.
Tumekuwa masikini katika upande wa kuelewa mazingira yetu kiasi leo ni wageni wenye utaalamu katika kuelezea maisha na tabia za wanyama wanaoishi kwenye mbuga zetu kiasi sisi tumebaki wabeba vifaa ya kupigia picha na wapelekaji wa watu porini.
Tumeshindwa kufahamu tabia za wanyama na faida zao  kiasi tunawaona kama kikwazo kwetu badala ya kuwa ni tija yenye thamani kuu. Leo hii tukimuona mbwa tunaokota jiwe kumpiga bila sababu wala fikra wakati mbwa huyo anaweza kutumika kutambua magonjwa kama Cancer katika mwili wa binadamu, ama kutambua kuwepo kwa dawa za kulevya ama silaha.
Leo hii wanasayansi wanamsoma Inzi kutambua uwezo wake wa ajabu wa kuweza kuruka na kutua katika dari ili waweze kuigiza katika mifumo ya kuendesha ndege lakini kwangu wewe na mimi tunamuona si kitu. Leo hii wanasayansi wanamsoma mjusi kutambua uwezo wake wa kutembea kwenye kuta na glasi ili waweze kutengeza gundi lakini kwangu mie na wewe tunaona bora tumpige fagio afe. Leo hii wataalamu wanatambua kwanini Simba dume halei watoto wa kambo kwangu mimi na wewe hii ni hadithi.
Leo hii tunachoona ni barabara tu bila kufikiri kuwa barabara si lami tu ilotandazwa bali ni mfumo mzima wenye taathira kuu kila inapopita. Kuhifadhi mazingira ni jukumu la taifa zima na kuwepo kwa mbuga iwe ni chachu ya kutambua umuhimu wake kuwepo pale.
Leo hii wanyama kama Simba wameingizwa kwenye Listi ya wanyama watakaopotea baada ya miaka michache inayokuja kutokana na shughuli za binaadamu kuhamia katika mazingira yao hivyo kuzuia mihamo yao kutoka katika familia walizozaliwa kwenda kuhamia kwenye familia nyengine ili kuepusha kuzaliana wenyewe kwa wenyewe na hiyo kusababisha madhara ya uzaofinyu (Inbreeding). Kwa hili hata sisi binadamu tunaweza kujifunza lakini kwasababu ya umasikini wa fikra hatulioni hili.
Suala la kusema mahitaji ya wanyama yamewekwa mbele zaidi ya binadamu kwanza tukumbuke kuwa binadamu ni mnyama pia. Na katika mfumo mzima wa maisha wanyama wote wana mchango maalumu katika kuwepo kwao. Kutokana na ubinafsi wa binadamu na kujifanya kuwa na akili nyingi tumeharibu sehemu nyingi za mfumo huu kiasi taathira zake zimekuwa zikituangamiza sisi wenyewe.  
Tanzania tumebarikiwa kuwa na utajiri asilia ambao ni bora kuliko faida ya hiyo barabara. Tunachotakiwa ni kufahamu utajiri huo na kuuthamanisha ili tuweze kupata tija. Wenzetu wa nje sio kwamba wanatukwaza bali kutokana na ukosefu wa elimu na kutoona mbali tulionao wanatuonea huruma tukija kupoteza utajiri huu tutakwenda kwa nani.
Wazungu waliwaua wanyama wenye kuwinda na kuwindwa kwenye nchi zao baada ya miaka mia ndio wakaona taathira waliyofanya na sasa wanatumia mabilioni ya pesa kurudisha wanyama hao ili wabalance ile natural order iliokuwepo. Leo hii kwenda kutazama ndege kipanga inabidi uombe leseni na hupati leseni hiyo bure ni lazima watizame historia yako, sie kwetu bure tunawaona wasumbufu wanaotuibia kuku. Dar es salaam kulikuwa na ndege kila aina miaka ya tisini leo hii waliobaki ni kunguru je unaijua sababu?
Watanzania tuache maneno ya kisiasa penye kuhitajika utaalamu..inaonyesha tuko tayari kuuza shamba kwa mlo wa leo tu..
Mungu Ibariki Tanzania na Tupe ufunuo katika fikra zetu.
Mdau Mwanafunzi.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    safi sana mdau mwanafunzi umeeleza vizuri sana nakupongeza inaonesha ni jinsi gani uko maini sio kutoa maoni ya kuripuka tu nakupa hongera sana.. il atatizo ni viongozi wetu wameshakula hela na wala hawasikii la mtu yaani viongozi wetu ni sawa na vichaa wa ulaya, hivi mr kikwete huwa anasoma hata news? no nadhani huwa anaangali tv za mashindano ya kil award, miss ilala, miss vodacom na kujuwa kiongozi gani wa chadema kakamatwa, useless mr kikwete na watanzania wote kwa jumla..

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Kupitisha njia kwenye mbuga ya wanyama sio suala la busara hata kidogo na hili litakapotendeka tutakuja kulaumiwa na na kizazi chetu kwa kosa tutakalolifanya leo hii

    ajabu nchi hii kuwa iko na wasomi wa kuweza kuona mbali na wakaweza kutaka kufanya suala hili kama vile nikusema idadi kubwa ya watanzania hawajakweda shule, naliita suala la kitoto kabisa kupitisha njia katika mbuga na athari zake ni kubwa kuliko wanavyofikiria wao

    naomba wahusika wenye kauli katika nchi hii watupie mbali suali hili la kitoto

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2011

    Asante sana bwana mwandishi kwa makala yako nzuri, mimi si mtaalam wa wanyamapori lakini hii makala imenisaidia sana kuelewa kibagaubaga upande mmoja wa shilingi.

    Sasa inabidi tujiulize hao wanaosema ijengwe wamepima faida na hasara zake? Na ni nini hasa kinasababisha eneo hilo liwe special kiasi hicho. Mbona huku kwetu matombo kuna mazao mengi lakini tunashidwa kuyapeleka sokoni kwa ajili ya barabara mbovu, naomba nisaidiwe sababu kuu ya kusisitiza kuhengwa barabara huko mbugani wakati kuna maeneo mengi hayana barabara?

    Nawakilisha

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2011

    Umesema vyema na ninakuunga mkono kwa uchambuzi yakinifu. Kuwepo kwa barabara katika mbuga hiyo ama kweli kuna athari nyingi kwa wanyama wote tukiwapo sisi wenyewe. Wewe kijana unajua kujenga hoja na ninaikubali hii hoja yako kama ilivyo. Tunahitaji wanafunzi wenye uchambuzi yakinifu kama huu kusaidia taifa letu na siyo mijitu kubwabwaja miono yao isiyo na urefu wa miaka mia ijayo.
    mdau kutoka Ufini

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2011

    Naungana mkono na wadau hapo juu. Mimi si mtaalamu wa mazingira lakini aina haja ya kuwa na uataalamu kugundua mdhara ya barabara mbugani. Tusiende mbali, angalia mikumi jinsi watu wanavyotupa ovyo taka na jinsi wanyama wanavyogongwa. Nchi nyingi duniani wamehathirika na suala la kupitisha barabara mbugani iliwemo kuongezeka kwa logging na uwindaji haramu leave aside madhara aloeleza mdau hapo juu.

    Swali langu wanaharakati wa mazingira mko wapi? Kwa nini hatuitishi maandamano tunakalia kulalamika pembeni.

    Hii nchi katika miaka 20 ijayo itageuka gofu maana si jangwa. Na hii tutaishuhudia wenyewe si kizazi kijacho.

    Yes we are poor but why shouldn't we have something to proud ourselves with.

    Hamuoni baadhi ya nchi kama seashels zimekuwa kivutio kwa watalii just because of natural beuty? What do we have if even the natural reserves are about to be destroyed?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2011

    Nakuunga mkono mdau.

    na mimi kuna siku nilituma post moja kwa michuzi akaibania, ni kuhusu kiwanda cha soda ash pale lake natron. Mimi nafikiri hiyo ndo sababu kubwa ya kujenga barabara ya lami. Lakini tunasahau huo uharibifu wa mazingira utakaosababishwa na 1, ujenzi wa hicho kiwanda, 2. kemikali zitakazotoka kwenye hicho kiwanda.

    Athari nyingine kubwa kwa kiwanda kuwepo pale ni kuwa hawa lesser flamingo hawataweza kutaga mayai yao na kuendeleza vizazi vyao, sababu lile ndo ziwa pekee kwa tanzania wanalotumia hawa kwa mazalio yao. Baada ya hapo nafikiri na utalii nao utakuwa umeisha kwa upande ule.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2011

    Madaraka ajiulize tuu kwanini Marehemu baba yake hakujanga hiyo barabara pamoja na kuacha utajiri wote wa nchi hii ubaki kama ulivyo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2011

    jana nilimuunga mkono makongoro kwa wapeeee wapeeee vidonge vyaoooooo....!!lakini wewe umekuja na hoja za kunikuna zaidi. nilichopata kwako ni kwamba faida za barabara zitatuondolea sifa tuliyobakia nayo tanzania (nature). Basi tusubiri jibu la makongoro kama ata "hit back...!!"

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2011

    Serengeti ni sehemu muhimu ya kiuchumi kwa asilimia ndogo ya Watanzania. Wenye kufaidika na Serengeti ni wenye mahoteli, makampuni ya utalii, wafanyakazi wa mahoteli, wafanyakazi wa makampuni ya utalii, na serikali. Watalii wengi wanalalamika kwamba wanyama ni taabu kuwaona huko Serengeti na sio kama vile wanavyona kwenye luninga. Serengeti ni kubwa sana, sasa kama wanyama wamehama sehemu moja kwenda nyengine ni vigumu kwa watalii kuona hao wanyama. Je watalii wangapi wanaokwenda Serengeti kwa mwaka? Je kwanini ijengwe barabara sehemu ambayo watumiaji ni kidogo. Serengeti hakuhitaji barabara kwa wakati huu. Barabara zijengwe sehemu kwenye mahitajio muhimu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2011

    Woooote hamjui mnachokiongea. Ni uzembe tu wa watatnzania lakini kama si uzembe barabara hiyo inaweza kujengwa na wanyama wasiathirike. Kwani huko mbugani magari hayaingii kupeleka watalii? Mbona Ngorongoro kuna magari mengi sana yanaingia kule kila kukicha lakini wanyama hawafi? Mbona pollution iko hata mijini na kuna wanyama kama mbwa, sungura, n.k lakini hawafi? Je mbona mijini kuna zoo mfano pale Ikulu ya Tz na wanyama hawafi? Mbona Australia Kangaroo na wanyama wengine wapo mijini na hakuna anayekuafa kwa ajili ya pollution? Acheni kutrumiwa na wakenya mkaididimiza nchi yenu. Wakenya na waganda wanaogopa kupoteza bishara hasa za magari yanayopitia kwao ambapo hiyo barabara ikijengwa hayatapitia tena kwao. Mbona wao wanajenga Airport hadi kwenye mbuga za wanyama? Barabara hiyo ni muhimu sana kwa wananchi wa musoma na maeneo mengine. Mimi ninaamini kabisa hiyo barabara ikijengwa ikawekewa sheria kali, barabara inaweza kupita bila kuathiri wanyama. Kwa mfano: kukiwekwa surveilance camera kila baada ya umbali fulani, kukawa na control room ambayo itahakikisha anayeendesha gari vibaya anakamatwa na kupigwa faini kubwa na pia kuifunga hiyo barabara kipindi wanyama wanahama, ninaaamini hakuna kitakachoharibika. Fikirieni kabla ya kuongea. Mimi namuunga mkono Makongoro asilimia mia kwa mia.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2011

    siwajenge tu underground, hilo litaskuwa suluhisho la kweli

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2011

    Ninyi msiosoma taarifa mbalimbali ndio hamjui kinachoendelea duniani. Hayo maneneo aliyoandika huyo anayejiita mwanafunzi yalishaandikwa na Wakenya na waganda mda mrefu wakati wanapiga kampeni hiyo barabara isijengwe. Alichofanya huyo mwanafunzi ni kutafsiri tu kile walichoandika wakenya hao na waganda kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili. Na unaweza ukute ni Mkenya aliyeomba msaada wa mtu amtafsirie. Hata hiyo ramani walishaitengeneza mda mrefu sana. Wakenya wanafanya lobbying ya hali ya juu kuhakikisha hiyo barabara haijengwi. Wanaogopa competition. Kuna biashara nyingi watapoteza. kwanza watalii wataingia kule kiurahisi bila kupitia Kenya, pili magari ya Tanzania ambayo yanapitia Nairobi wakati wa kwenda musoma hayatapitia tena, tatu magari ya Rwanda ambayo yantoka bandari ya Mombasa kupitia uganda hayatapitia tena huko na badala yake yataitia Serengeti. Mimi namuunga mkono Mkaongoro.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2011

    Angalizo. Nina wasiwasi na umakini wa wachangiaji karibu wote, wametumia jina la Makongoro badala ya Madaraka. Wote ni watoto wa Mwalimu Nyerere na Mama Maria lakini wakati Makongoro ni mwanasiasa nduguye Madaraka ni mjasiriamali na mtafiti.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2011

    watanzania wenzangu tufikirie kipi bora katika maisha yetu,tukichukuria nadhalia ya evolution wanyama wote wana uwezo wa kubadilika kutegemeana na mabadiliko ya mazingira ikiwemo binadamu.hatuwezi kuanza kufikiria faida ndogo ya inzi na mjusi kama wenzetu mmoja aliyesema na maendeleo ya watanzania.ujenzi wa barabara hiyo bado ni muhimu kwa faida ya watanzania wa kaskazini mashariki na taifa kwa ujumla.tuache kufanyia kazi nadharia zilizopitwa na wakati.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2011

    Semeni tru Kikwete anajenga hoteli huko wengine twajua. Michuzi bania hii

    ReplyDelete
  16. Mimi wadau nataka mnielimishe kwa nini Kwenye Mbuga ya Mikumi ilijengwa lami,au ile lami ilikuwepo kabla haijawa Mbuga?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2011

    "In accepting the trusteeship of our wildlife we solemnly declare that we will do everything in our power to make sure that our children's grand-children will be able to enjoy this rich and precious inheritance." - Mwl. Julius K. Nyerere

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2011

    Asante mdau kwa mawazo yako mazuri. Lakini kwa maelezo hayo hayajabainisha kuwa eti barabara ikijengwa Serengeti eneo lililopendekezwa, eti athali hizo zitaathili wanyama na hatimae kutoweka! Nasema kwa sababu zifuatazo:
    i) Katika uchambuzi wako hutatueleza ni mbuga ngapi ambazo barabara hupita ikawa hapa kwetu Tanzania, Afrika, na duniani.
    ii) Kati ya hizo mbuga zenye barabara, ni ngapi ambazo wanyama wake wametoka imebaki tupu.
    iii) kama hiyo haipo na haijawahi tokea mpaka sasa, kwa nini IFIKIRIWE kutokea Serengeti tu?
    iV) Barabara mbadala (alternative route) ulioonyesha kwenye ramani nayo inapita Mbuga ya Serengeti (Kutoka Bunda-Ramadi) tena mahali penye ziwa (fresh water) ambalo ndio chanzo cha uhakika wa maji kuliko mto wowote! Je huoni hapo ni kuluka mkojo kisha unakanyaga mavi?
    v) breeding sites: sijaelewa kama barabara itapita kwenye breeding sites au ni mapito ya Wanyama tu. Pia tuzingatie kuwa sehemeu yoyote ya mbuga ni mapito ya wanyama. Hivyo, barabara kujengwa, hakutazuia wamyama kutopita. Ila sehemu za mazalia, nathani nimeepukwa na kwa hali hiyo, wanyama wataendelea kuzaliana.
    vi) Umesema vyema kuwa wanyama hutegemeana (predators). Ni kwa msingi uo huo, nasi tutegemeane kwa kutumia sehemu ya mbuga.
    vii)n.k (baadae)
    Niishie kusema, kuwa kwa mawazo yangu, sijaona tatizo la ujenzi wa barabara. Ila ni wajibu kubaini athali (impacts) zinazoweza kushababishwa na ujenzi barabara hiyo au hata nyingine yoyote ile na kutafuta njia ya kuzikabili (remediation) na wala si kutojenga.

    Nawasilisha-Mwanafunzi Pia

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 07, 2011

    Mimi kama Ningekuwa kikwete basi Ningetafuta mapesa na kujenga barabara ya daraja juu kwa juu moja kwa moja serengeti yote. Hiyo inaweza kuwa pia kivutio zaidi kwa wasafiri na watalii. Waugwana mnaonaje hilo...

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 07, 2011

    Hoja zote ni muhimu na pande zote kuna faida na hasara. Jambo muhimu hapa ni kigezo gani kitachotumika kuamua jambo hili ambalo linaguza hisia na maslahi ya wengi sasa na hasa kizazi cha baadaye. Tuitishe mdahalo wa kitaifa ili tupime hoja zote mbili - wanaounga mkono na wanaopinga washindane kwa hoja ili na wananchi wengine wa kawaida kwanza waelewe kinachoendelea, na pili nao waamue waunge mkono hoja ya upande gani, maana ni suala linalowagusa watanzania wote. Wanaharakati wa mazingira na waandishi wa habari hasa wa TV mko wapi??? Huu ni wakati wa kutetea mnachokiamini! Kama kuna kampeni chafu kutoka kwa jirani zetu, basi tuzishinde kwa hoja, kila mmoja wetu atumie nafasi yake kutetea anachokiamini!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 07, 2011

    Natural selection is the process by which biologic traits become more or less common in a population due to consistent effects upon the survival or reproduction of their bearers. It is a key mechanism of evolution.

    The genetic variation within a population of organisms may cause some individuals to survive and reproduce more successfully than others. Factors which affect reproductive success are also important, an issue which Charles Darwin developed in his ideas on sexual selection.

    Natural selection acts on the phenotype, or the observable characteristics of an organism, but the genetic (heritable) basis of any phenotype which gives a reproductive advantage will become more common in a population (see allele frequency). Over time, this process can result in adaptations that specialize populations for particular ecological niches and may eventually result in the emergence of new species. In other words, natural selection is an important process (though not the only process) by which evolution takes place within a population of organisms. As opposed to artificial selection, in which humans favor specific traits, in natural selection the environment acts as a sieve through which only certain variations can pass.

    Natural selection is one of the cornerstones of modern biology. The term was introduced by Darwin in his influential 1859 book On the Origin of Species,[1] in which natural selection was described as analogous to artificial selection, a process by which animals and plants with traits considered desirable by human breeders are systematically favored for reproduction. The concept of natural selection was originally developed in the absence of a valid theory of heredity; at the time of Darwin's writing, nothing was known of modern genetics. The union of traditional Darwinian evolution with subsequent discoveries in classical and molecular genetics is termed the modern evolutionary synthesis. Natural selection remains the primary explanation for adaptive evolution.

    Davi V

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 07, 2011

    We Anonymous wa June 07, 3:02 AM ,Mwanafunzi ana blogu zake ukitaka zitembelee sio mtu wa kukopi au kutafsiri ni original katika mada zake.. nenda http://kamerayamwanafunzi.blogspot.com/ au http://i-quantumphysics.blogspot.com/ utaona vitu vyake sio porojo za siasa unazotaka kutuletea..

    mdau aliyeguswa..

    ReplyDelete
  23. Kwakweli hata mimi malalamiko ya Bw. Nyerere yalinishangaza sana na sikumuelewa kama analijua swala hili kwa undani au alikurupuka tu.
    Ukiangalia kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania utaona kuwa njia mbadala ina manufaa zaidi kwani ina kilometa 40 zaidi na pia inapita sehemu ambazo kuna watu na vijiji vingi zaidi hivyo kuwafikishia maendeleo kwa ukaribu zaidi kuliko ile iliyopendekezwa na kwa upande mwingine hii njia mbadala World Bank wamekubali kuifadhili kwa asilimia 100 (100% financed by World Bank) wakati hii nyingine hawako tayari na itabidi tuigharamie kutoka fedha za walipa kodi kitu ambacho kitaongeza matumizi toka bajeti yetu

    Kwanyie mlioko nje ya nchi naomba msipende kuchangia kwa kuona sisi tuliopo nyumbani hatujui kinachendelea huko kwenu, ukweli ni kwamba nyinyi mnataka Africa iwe kama huko lakini huwezi fuga Simba au Chui au hata Nyati mjini hilo haliwezekani kwahiyo kama huko mnapishana na Kangaroo mjini hiyo ni huko huku mazingira na hata wanyama wenyewe ni tofauti sana

    Mwisho nashauri kwa maendeleo ya Watanzania wengi watu wote ni bora tuunge mkono njia mbadala (Alternative root) ambayo itafadhiliwa na WB na kuwafikia watu wengi zaidi kuliko hiyo itakayo haribu ikolojia na pia kuwa na manufaa kwa watanzania wachache kwa gharama za walipa kodi wa Tanzania

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 07, 2011

    Namuunga mkono mwanafunzi na wanaosema kuwa ni Wakenya wanaopinga ujenzi wa barabara ana mawazo mafupi sana hana upewo wa kuangalia maisha yetu ya mbele. Suala la ujenzi wa barabara ni suala la maendeleo yetu na sio ya Wakenya au Waganda, wao wana matatizo yao. Sisi kama Watanzania ndio inabidi tufanye uamuzi mzuri wenye lengo la kuendeleza nchi yetu na ujenzi huo utaturudisha nyuma. Kuna alternative southern route badala ya kujenga ndani ya mbuga za wanyama.

    John Kijiko

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 07, 2011

    AISEE CONFUSION INABIDI JOPO LA WATAALAMU LIKAE KAMA KAMATI KUPIA FAIDA NA HASARA KISHA UFANYIKE UAMUZI YAKINIFU

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 07, 2011

    Mnaotaka hiyo barabara icjengwe hamieni Kenya lakn cc wanaMusoma tunamuunga mkono JK 100% aanze ujenzi mara moja kabla hajaondoka, mnayohaki ya kupinga sababu hamjui adha ya barabara tunayoipata, hiyo environment impact assessment imefanywa makusudi ili ionekane kutatokea madhara makubwa kwa natural resources ili waKenya waendelee kutufanya shamba lao la bibi lakudumu kitu ambacho kwa sasa hatutokubali kabisa kiendelee kufanyika. manufaa kiuchumi yanayopatikana kwa sasa kwa nchi huwezi linganisha na yatakayopatikana baada ya barabara hiyo kujengwa kwa kutumia akili za kawaida tu.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 07, 2011

    Hivi jamani, Mikumi imepita barabara kubwaa na wanyama wapo tele. Selou imepita reli ya tazara na wanyama wapo tena unawaona wakati unapita na treni reli imejengwa toka mwaka 1972! Hata ukienda namtombo huko Mkuju river utakuta kampuni ya Mantra inachimba Uranium hao wanyama wa Serengeti wako delicate kiasi gani kushinda hao wa mfano selou ambayo no mojawapo ya world natural heritage?

    Mmenikumbusha wimbo wa Pr. jay ndiyo mzee hasa huyo jamaa wa wapewape vidonge.

    Wabongo msiwe wasikilizaji na washangiliaji wa hoja za majirani, hebu na sisi tufikirie kwa maslahi yetu wenyewe.
    Hebu angalia ndugu zetu wanvyofanywa kwenye migodi, lakini akija mtu akawadangaya kidogo watanzania wote tunawageuka ndugu zetu na kuwaona wakosaji.

    Ona mnvyorubiniwa na kanga, bia na visenti wakati wa kipindi kifupi cha kampeni na kuasahau kipindi kirefu cha tabu kitakachofuata.

    No one ca free your minds than yourself on top wasomesheni na watoto wenu basi

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 07, 2011

    Wewe ni mkenya lengo lenu ni kutuharibia kila kitu,mmeshiriki kuua ATC na kuanzisha precision air kimgongongo,mmeua general tyre haya yote mkishirikiana na wabongo waliofilisika uzalendo,ndiyo maana hatukushangaa kwa wakenya kukamatwa kwenye vurugu za Arusha,tuachieni nchi yetu,barabara hiyo ni muhimu sana kwa uchumi wetu,mbona wanyama wa mikumi hawafii,mbona na nyie kwenu kuna mbuga iko mjini tena karibu na airport,acheni hizo !!??

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 07, 2011

    Huyu ni mwanafunzi je hapo atakapo fuzu atakuaje? Hii ndio inayotakiwa funika bovu. Ona alivyo mvua nguo mtu mzima. Bila ubishi hapa madaraka lazima achuchumae tuu. ASANTE SANA STUDENTI

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 07, 2011

    Barabara ni sehem ya maendeleo lakini ikumbukwe maendeleo ya mwanadamu ndio sababu kubwa ya uharibifu wa mazingira uliopo leo duniani. Hakuna haja ya kubishana lakini wahanga wa kubwa wa madhara ya kimazingira yanayotokana na maendeleo ni mataifa yaliyo endelea fuatilia utaona hilo liko wazi. Barabara itakayo jengwa ni lazima itaaacha athari za kimazingira, tusitoe mifano ya kimzaha kwa mfano zoo ya ikulu ya Dar utaifananishaje na uoto na wanyama wa asili walioko katika mbuga ya serengeti? inasikitisha sana kuona watanzania tena wenye haiba ya juu katika jamii hawajui tofauti ya zoo na maeneo asilia wanayo ishi wanyama. Kama Australia kuna zoo kwann wao wanakuja serengeti kumwona simba? Tuchangie kwa hoja.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 07, 2011

    Hivi ni kweli hoja yoyote nzuri haiwezi kuchangiwa na Mtanzania? Mbona tunajidhalilisha jamani watanzania? Kusema huyu aliye changia hapo juu kuwa ni m Kenya au Mganda tunarudi kulekule. Ukweli unabaki palepale kuwa ujenzi huu wa barabara kupitia Serengeti una athari za kimazingira na umepingwa na wapenda mazingira wengi ulimwenguni kote na sio Kenya au Uganda kama baadhi ya wachangiaji wanavyo taka kutu sadikisha bofya hapa www.savetheserengeti.org/issues/stop-the-serengeti-highway/ au hapa blog.mongabay.com/.../activism-alternatives-to-the-serengeti-road/. Swala hili si la ki nadharia ni swala nyeti na lina athari kwa ulimwengu wote unaopenda asilia. Ni juu ya kila mwanadamu kupenda mazingira kuyaharibu kwa kisingizio chochote ikiwamo maendeleo ni mtazamo potofu.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 07, 2011

    HATUTAKI BARABARA ITAKAYO HARIBU URITHI WETU. WANA SIASA MME TUMALIZIA MADINI YETU INATOSHA, SASA MTUACHIE WANYAMA WETU WA ASILI KWA AJILI YA VIZAZI VIJAVYO.

    ReplyDelete
  33. hacheni utoto, kwan kujenga barabara ni vibaya?????????????

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 07, 2011

    jamani kwani lami lazima uende kasi? lakini hata hivyo mbona hamsemi kuhusu hicho kiwanja cha ndege wanachotaka kujenga hao wakenya karibu kabisa na mlima kilimanjaro.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 07, 2011

    Huyo student ame-copy na ku-pest.Tatizo lenu wachangiaji wengi hamsomi makala mengi huyo amechukua makalailiyoandikwa muda mrefu sana na Wakenya wakitetea barabara hiyo isijengwe, ndiyo anaiweka hapo kutetea uozo wa kukataa kusijengwe barabara.Bila shaka msomi na wanayama pori na msomi wa mambo ya uchumi hawawezi kupikwa pamoja kwa sababu kila mmoaja atatetea maslahi yake yalipo pasipo kuangalia maslahi ya wengi.

    Madaraka, ameangalia sana suala hilo kiuchumi na kijamii jinsi inavyoathiliriwa na ubovu wa kukosa miundo mbinu imara.Huyo anayejiita mwanafunzi ameangalia kitumbua cha ajira yake kwa sababu ameshindwa kuelewa kuwa miundo mbinu ya barabara ikiimarika inaleta faida kwa binadamu na kwa wanyama pia.Tatizo la wachangiaji wengine ni kushabikia zaidi kuliko kutafakari kwa kina kile kinachoongelewa.kama watalii wanapelekwa na magari huko sijui hayo magari ni tofauti na yale yatakayokuwa yanapita kwenye rami au vipi??

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 07, 2011

    We mwanafunzi inaonekana umekaa sana ughaibuni wewe, kama unakaa Tanzania mambo yako safi hujui maisha ya mlalahoi. Yaani unajali maisha ya wanyama kuliko ya binadamu???

    Redo your SWOT analysis please...

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 08, 2011

    Sikatai kua barabara ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na pili naomba kuunga mkono mwanafunzi, kila mnyama (binadamu pia) ana nafasi, kazi na makazi yake katika ecosystem nzima, wanyama pori habitat yao ni pori, kuleta barabara katikati ya Serengeti kutavuruga ecosystem kama mwanafunzi alivosema lakini pia kuna kitu kinaitwa Environmental impact assesment (EIA) ambapo wanaangalia sehemu mbalimbali ambazo wangeweza kujenga hiyo barabara and they make a cost-benefit analysis, choosing a route with less impacts while catering the same needs and that is what was needed to be done in Serengeti, the World bank is ready to help with the EIA studies on different routes
    hata kama hii idea ya kutojenga barabara inapigwa na wakenya na uganda kwasababu ya maslahi yao it doesnt not take away the truth that building the proposed road is a huge mistake and there will be huge impacts so the thing to do here is study other alternatives and then go with the one with less impacts
    nawasilisha
    Mwanamazingira

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 08, 2011

    Say NO TO SERENGETI HIGHWAY kama wewe ni mtanzania wa kweli na unaipenda nchi yako...msiingizwe kwenye siasa angalieni ukweli. Kama kuna wafadhili watakaotoa msaada kwa route mbadala ya nini kung'ang'ania hiyo ya Serengeti?Watanzania amkeni acheni kufuata siasa zisizo na maana jenga nchi yako sema NO TO SERENGETI HIGHWAY

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 09, 2011

    Ebwana eeh mi huyu mwandishi kwa kweli na msifu sana na ingawa mimi si mtaalam sana wa masuala ya wanyama lakini pia napinga kuwepo kwa hiyo barabara.
    unajua ndugu mwandishi watanzania wengi sana wana akili na upeo wa kuyaona ya nje lakini most of us hatupewi kipaza sauti tukasema yetu.
    kwa mfano we muangalie huyu mdau aliyeelezea haya maoni yake na alivyojua kuyachambua, yaani mi naweza kusema mshikaji ni msomi wa kufu mtu(hata kama hajafika shule) na alichokisema kinatusaidia wote.
    Tuwe na utamaduni wa kuwasikiliza watu wa chini na sauti zo jamani eeeeeeeeeeeh

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 11, 2011

    Bwana Michuzi & Wadau wengine;

    Katika kueleza mawazo, kunakuwepo maoni ya kihisia (emotional comments)na pia kuna maoni yanayojikita katika tafakuri, utafiti na pembuzi yakinifu kabla ya kuyaweka bayana.

    Hivyo: tukiangalia kwenye hisia:Hapa kuna suala la uzalendo, uraia, uhuru wetu kama nchi inayojitawala yenyewe bila kuingiliwa na nchi ye yote nyingine na mengineyo kama hayo. Wadau, mawazo ya aina hii hayana tija na ni budi tufikiri kabla ya kunena/kuyaweka wazi.

    Tafiti mbalimbali na pembuzi yakinifu zimeonyesha kwamba ukilinganisha faida ya kujenga barabara kuu ya kibiashara (Commercial Highway) inayokatiza Hifadhi ya Serengeti (SENAPA) NA athari za ujenzi huo; athari ni nyingi kuliko faida.

    Serikali yetu imesema sababu kuu za kutaka kuendesha mradi huo ni tatu: 1. Kuunganisha mikoa ya Arusha na Mara; 2. Kujenga miundombinu na kuongeza uchumi wa nchi; na 3. Kusogema huduma za jamii na maendeleo kwa wananchi wa vijijini waishio katika maeneo ambapo barabara kuu hiyo inategemewa kupita. (Angalia kwamba 'wananchi' si sababu ya kwanza wala ya pili - wao ni namba 3.!!)

    Ukiondoa sababu za kisiasa, barabara kuu hii ni sawa na kile wenzetu wakiitacho 'white elephant' (Tembo Mweupe): Nadra kupatikana (ni albino), gharama sana kumtunza, na hana faida zaidi ya kuwa 'tembo wa Mfalme' - ni wa maonyesho tu (for pomp and show only).

    Umuhimu wa barabara zipitikazo majira na misimu yote hususan vijijini ni jambo lisilokwepeka. Sasa kama Benki ya Dunia (World Bank) na Serikali ya Ujerumani kwa nyakati tofauti licha tu kukubaliana na Serikali ya Tanzania kuhusu umuhimu huo na kuonyesha nia ya KUFADHILI (si kukopeshs) Serikali yetu kutimiza azma yake ya kuwa na barabara hizo; huku SENAPA ikibaki na hadhi yake kama ilivyohivi sasa; NI KWA NINI Serikali inasuasua kutoa tamko la AMA kukubali ufadhili huo ama kutoa sababu za msingi kwa nini haipo tayari kupokea msaada huo usio na masharti?!

    Ukiingia katika kurasa za FaceBook ukatembelea 1. STOP THE SERENGETI HIGHWAY; 2. SERENGETI WATCH (savetheserengeti.org); ama 3. CLICK 'Like' YOU WISH TO SAVE THE SERENGETI - utaona kuna maelfu ya watu/asasi/azaki wakitoa maoni yao jinsi ambavyo uamuzi wa kujenga barabara kuu ya kibiashara kukatiza SENAPA kutakavyoiumiza si tu Tanzania, bali hata mazingira ya maisha ya baadaye ya Watanzania (wananchi) wenyewe!! Wengi walioandika kabla yangu wamekwisha kuzitaja - hivyo nisipoteze muda wenu muhimu.

    ILA: TUTAFAKARI TENA NA TENA. KUFANYA KOSA LA NAMNA HII HUWEZI MIAKA 20 - 50 HUKO MBELE WATOTO WETU/WAJUKUU WETU WAKASEMA 'WAZEE WETU WALITUACHIA LAANA HII'!! HAKUNA KITU KAMA 'BUTTON' YA KEYBOARD YA KUBOFYA 'UNDO'!! IT WILL BE CATASTROPHICALLY AND TRAGICALLY TOO LATE!!

    Bipin Vishani - Msasani Village
    e-mail: bipinvishani@gmail.com
    Facebook/bipin.vishani.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...