| Ja Rule akiwa amezingirwa na wafanyakazi wa 88.4 Clouds FM radio alipotembela Tanzania mwaka 2006 | 
Msanii wa Hip-hop  Ja Rule yuko lupango ambako alijipeleka mwenyewe katika gereza moja huko New York, Marekani, na  kuanza kutumikia adhabu ya kuwa kifungoni kwa miaka miwili.
Rapa huyu ambaye ameshafanya ziara Tanzania wakati wa Fiesta ya mwaka 2006, na ambaye jina lake halisi ni  Jeffrey Atkins,  alikiri makosa mwezi Desemba mwaka jana kwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria ndani ya gariu lake la kifahari, huku silaha hiyo ikikutwa imekwanguliwa namba zake za usajili. Tukio hilo lilitokea  kitongoji cha New York cha  
Ja Rule alijisalimisha mwenyewe gerezani hapo saa nne asubuhi siku ya Jumatano, kabla ya kupelekwa  
Katika miezi ya karibuni Ja Rule alikuwa anamalizia kurekodi albamu yake  mpya – ya kwanza katika miaka sita – inayotegemewa kuwa sokoni baadaye mwaka huu.


 
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...