Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa, akielezea hatua mbalimbali, zinazochukuliwa kuwaadhibu viongozi wabadhirifu wa mali za umma na utatuzi wa kero zinazowakabili ambazo zinakwamisha maendeleo yao wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mh. Fatma Mwassa,akiwahoji baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Kigugu, Kijiji cha Bwage , Kata ya Kanga, baada ya kukuta mti wa asili aina ya mninga uliokuwa kwenye shamba la Mkulima Mwajuma Malongo , umekatwa kwa ajili ya  magogo  ya mbao  bila ya kupata kibari halali kutoka Ofisi yake, Mkuu wa Wilaya huyo na Maofisa wake walikuwa njiani kwenda katika Kijiji cha Mziha, Wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa, akisoma Ujumbe wa Maandishi katika simu yake aliotumiwa na mmoja wa wananchi wa Kijiji cha  Kigugu, Kata ya Sungaji, zinazohusu kero mbalimbali ikiwemo ya Uchakachuaji wa vocha za ruzuku za pembejeo
Vibarua wakitelemsha gogo la mti wa asili wa mninga walilopakiza kwenye gari baada ya kutolewa kwa amri na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero  Mh. Fatma Mwassa ( hayupo pichani), baada ya kukuta umekatwa  kutoka katika   Shamba la Mkulima , Mwajuma Malongo ( hayupo pichani), bila ya kupata kibari halali kutoka Ofisi yake. 
Picha na mdau John Nditi


 
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...