Thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa mwaka 2010 ilishuka kwa asilimia 8.5 hadi wastani wa shilingi 1,432.3 kwa dola moja ya Kimarekani kutoka wastani wa shilingi 1,320.0 mwaka 2009. 

Thamani ya shilingi ilishuka kwa kiwango kidogo mwaka 2010 ikilinganishwa na asilimia 10.4 mwaka 2009, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya dola nchini pamoja na kuimarika kwa dola ya Kimarekani dhidi ya sarafu za mataifa mengine. 

Bei ya dola moja ya Kimarekani mwishoni mwa Desemba 2010 ilikuwa na thamani ya shilingi 1,453.5 ikilinganishwa na shilingi 1,313.3 mwishoni mwa Desemba 2009.

Wenye data za hali ilivyo sasa msaada tutani tafazali....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2011

    bwana hiyo fweza ilishabadilishwa we vipi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2011

    ..rekebisha hesabu zako: shilingi ilishuka thamani kwa asilimia 7.8 kwa viwango ulivyoviweka. Hiyo asilimia 8.5 ni ongezeko la thamani ya dola dhidi ya shilinigi.

    nawakilisha
    mujwaHuki

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2011

    Bank Of Tanzania rates for 9/Jun/2011

    Unit Buying - USD: 151,988.20
    Unit Selling -USD: 155,090.00

    Source http://www.bot-tz.org/

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2011

    Mimi sishangai kabisa na haya nilipata nafasi ya kukutana na kiongozi mmoja mtendaji wa juu sana serikali nikamuuliza na majibu aliyonipa kwa kweli hayakuwa ya kurithisha. Hii inachangai sana na kasumba yetu sisi wenyewe watanzania ya kujali na kuthamini vya wenzetu na kuacha vyetu vikiteketea, hivi kweli Tanzania tumekuwa hata vocha za simu tunanunua kwa dola ? shilingi inafanya nini ? nyumba unaopanda kwa dola ? kila kitu watu wanaona dola vdio mali wakati wengine hata nje ya nchi hawajawahi kufika kuitumia hiyo dola yenyewe ili mradi tuu wapate hizo dola moja moja kutunzia kitchen party !! Ulimbukeni unatumalizia nchi na serikali yetu na viongozi wetu wanayazibia mcho haya kutokana na faida zo wenyewe binafsi kwa kweli pesa ya nchi kushuka thamani si jambo la kufanyia masighara kabisa na ni kuteketeza kizazi kijacho. Sijui kwa nini watanzania hatuna mapenzi na nchi yetu na kizazi chetu ! anyway mimi nasikia uchungu sana sina la kufanay mana hili sio swala la mmjoja ni nchi nzima kuamua enough is enough but kutokana na uchu watu tulionao hakuna ataekubali kufanya hivyo, haya basi tuendeklee kukuza Dola na kuua shillingio. Mana hamuigi hata mfano wa KEhnya tuu hapo jirani jamani khaaaa !! inakera kwa kweli na bado mpaka tuitaaenda kununu mikate na hela kwenye matoroli kama Zimbabwe

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2011

    Dola kila siku inashuka thamani, iweje useme kuwa inapanda kuliko fedha za nchi nyingine? Na iweje shilingi ishuke thamani kwa dola ili hali dola inashuka kila siku?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...