Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu huria nchini wa kituo cha Bukoba wakijaribu kusoma soma muda mfupi kabla ya kuingia kwenye vyumba vya mtihani kufanya mitihani yao ya kumaliza mwaka wa masomo 2010/2011, mtihani huo ulianza jana na unafanyika kwenye jengo jipya la chuo hicho lililoko barabara ya kashozi iliyoko katika manispaa ya Bukoba. Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Bukoba
Home
Unlabelled
juhudi za kusaka nondozzz chuo kikuu huria bukoba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mandhari nzuri ya kujisomea, yaani nyie acha mimi sijafika huko bukoba au Mwanza lakini jinsi ninavyoona majabali yananivutia sana. Mimi sijui kwa nini wanahama kwao kuzuri namna wanakuja Dar kwenye misongamano na joto.
ReplyDeleteKisomo ni kitu cha maana, hata usome chini ya jiwe ili mradi elimu. Hii ndio tunatakiwa kutangaza tanzania. Elimu, elimu, elimu.
ReplyDeleteHapo mpaka ukute sehemu imeandikwa "NO SCHOOL AHEAD" ndo unachana na mambo ya shule
ReplyDeleteHapo zamani Bosi fulani kutoka Kanyigo alitaka kujenga hoteli miaka ya 85 hivi sijui kilitokea nini mpaka sasa ndo kama ilivyo hivyo
ReplyDeleteNami nilisoma BA huko Open univ, na kutumisa sana Teknohama na kujiwekea nidhamu ya kusoma kila wiki. Shule ya OUT inapanua uwezo wa kuchanganua mambo na kuelewa mambo mengi sana. Nimesoma Masters Univ of London, UK, na ilikuwa kama kumsukuma mlevi kutokana na uzoefu wa kudima Open. Kazeni buti, shule ya Open Univ iko juu sana
ReplyDeleteMdau
zenj
Safi sana hasa kwa kutambua ile BIASHARA haina nafasi tena katika dunia hii
ReplyDeleteWewe anonymous wa 04:46:00 unatafuta uchokozi wewe; utani wa ngumi huo. Biashara ipi hiyo unaongelea hapa? Mh;haya wee.Naamini wenyewe wamepata ujumbe. Tunawatakia mtihani mwema wadau
ReplyDelete