Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ramadhan Abdulla Shaaban amewateuwa wajumbe  11  wapya wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (State University of Zanzibar - SUZA). 

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Mwanaidi Saleh Abdulla Waziri Shaaban amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mwaka 1999 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kifungu cha 12(d). 

Walioteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza hilo ni Mh Said Mohd Said Mwakilishi kutoka Baraza la wawakilishi,Dkt Narman Saleh Jiddawi kutoka Taasisi ya Sayansi ya Bahari,Bwana Simai Mohd Said Mfanya Biashara,Bi Amina Khamis Shaaban Katibu Mtendaji Tume ya Mipango,Bwana Khamis Mussa Omar Katibu Mkuu Ofisi ys Rais Fedha ,Uchumi na Mipango na Bi Mwanaidi Saleh Abdulla Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali .

Wengine ni Dkt Zakia Mohd Abubakar Kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),Bwana Mmanga Mjengo Mjawiri kutoka SUZA, Bwana Maulid Omar Haji kutoka SUZA,Professor Mustafa Roshash Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar na Bwana Mtumwa Ali Ameir Mwenyekiti wa Serikali ya Wanafunzi SUZA. 

Aidha Bwana Hassana Nassor Moyo ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo. 
Uteuzi huo umeanza toka tarehe 15 juni,2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...