Mambo vipi brother Michuzi,

Natumaini uko salama. Lengo la email hii ni kuitambulisha service inayotuwezesha sisi kama Watanzania kuwa-analyse wabunge wetu. Mimi naitwa Nick Masao na profession yangu ni software development. Niko passionate na nchi yangu na ninakerwa na ufisadi, uzembe na hali ilivyo nyumbani na tunapoelekea kwa kweli. Kwa sababu sina namna ingine ya kusaidia, basi nikaona nitengeneze hii service ambapo mwananchi yeyote anaweza kuitumia kupiga kura kuhusu utendaji wa mbunge wake na pia kumpa maoni kuhusu nini anaona kinaweza kubadilishwa ili kuimprove mambo, au kumpongeza kwa pale ambapo anaona mbunge ni mchapa kazi. Inaitwa Tathmini na inapatikana kupitia
http://www.tathmini.com

Tathmini inawawezesha wananchi at least kufanya kitu ambacho kinaweza kuwa na mchango in the long run. Lengo langu ni kwamba baada ya muda fulani kama watu watarespond vizuri, basi tutacompile reports na
kumtumia kila mbunge aone ni kura ngapi positive alizopata na ni ngapi negative alizopata na pia maoni gani wananchi wametoa kwake.

http://www.tathmini.com/Pages/Details/2/lowassa-ngoyai-edward

http://www.tathmini.com/Pages/Details/3/chenge-john-andrew

Natanguliza shukrani,

Nick Masao
+255784653050 - Tanzania
+2316409442 - Monrovia
Twitter: @nickmasao
www.arushasoftware.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2011

    Well done kijana. Huu ndio ubunifu tunaoutaka na sio kutuwekea mambo ya ushabiki wa timu za wenzetu.

    ReplyDelete
  2. GOOD IDEA............ILA TU NINAOMBA SANA USIRUHURU MATUSI, SABABU NINAJUA KUWA KUNA WACHAFUZI WAKIINGIA HUMO NDANI, ITAKUWA NOMA..NA UTAPOTEZA WASOMAJI...CHONDE CHONDE SANA USIRUHUSU MATUSI KAKA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2011

    Hongera sana kaka..

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2011

    Ni kweli hili ni wazo zuri sana litamuwezesha kila mtu kuweka mambo hadharani yanayomuhusu mbunge wake,kama ni mazuri ataona na kama ni mabaya atatafuta njia ya kurekebisha.Kama alivyosema mdau hapo juu haileti maana kuona globu zetu ziko bussy kuleta upuuzi wa mabonanza na kushobokea timu za kigeni wakati nchi inaangamia !!Wananchi wamejisahau ktk shughuli za kijinga na mabonanza wakati hali ya nchi ni mbaya sana.Hongera kijana tupo pamoja na wewe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2011

    beautiful idea kaka! ila manage maoni hayo kwakutoa yanayo faa na utakayo yaona yaweza kua na positive impact!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2011

    good job....ungeweza kuongezea na wasifu wao (CV/ resume) kama ukipatikana itakua rahisi kwenye kutoa ushauri zaidi katika maeneo wenye utaalam nayo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...