Washiriki wa Miss Tabata 2011 wakiwa mbuga ya wanyama ya Mikumi leo 
 Miss Tabata wakiwa ndani ya basi lao
Washiriki wa Miss Tabata wakiwa Mikumi


Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Miss Tanzania kesho itatembelea  kambi ya Miss Tabata iliyopo Da’ West Park, Tabata. Kamati hiyo ikiongozwa na Mratibu wa Vodacom Miss Tanzania Hashim Lundenga itawafunda warembo hao kabla ya kushiriki kwenye kinyang’anyiro hicho siku ya Ijumaa.

“Tutaongea nao ili kujua uwezo wao kabla hawajapanda jukwaani kushindania taji. Pia tutawapa vidokezo vya urembo,” Lundenga alisema. Warembo 22 watashiriki kwenye kinyang’anyiro hicho ambapo bendi maarufu nchini African Stars “Twanga Pepeta” itatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo ni kivutio cha wengi  jijini.

Wiki iliyopita warembo hao walitembelea Mbuga ya Wanyama ya  Mikumi iliyoko Mkoani Morogoro. “Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kutangaza utalii wa ndani. Warembo walipata nafasi ya kuwaona wanyama waishio kwenye mbuga hiyo. Pia walijifunza mambo mengi ikiwemo kujua tabia za wanyama na ndege wote waliishio katika mbuga hiyo,” alisema mratibu wa shindano hiyo Joseph Kapinga.

Warembo waliosafiri na ambao watashiriki ni Marion Augustino (19),  Neema Marwa  (18), Catherine Julius (20), Lilian William (20), Godliver Mashamba (22) na Dorice Mutabingwa (21).

Wengine ni  Sweetlily Suleiman (21),  Maria John (21), Happyness Emmanuel (18), Cresensia Haule (20), Mariam Manyanya (21),  Agustina Mshanga (20), Nasra Salim (21),  Faiza Ally (19) na  Edina Mnada (21),  Angela Fortunatus (21),  Lucia Joseph (20),   Lilian Brayson (22),  Rita Mvungi  (21) na Willieth Wilson (22).

Miss Tabata 2011 imedhaminiwa na Dodoma Wine, Vodacom, Redds Original,  Integrated Communications, Paris Pub, Fabak Fashion, Freditto Entertainment, Chicken Hut, Travel Partners, Ben Expedition, Screen Masters, Sean Entertainment, Michuzi Blog, Anech Stationary na Vayle Springs Consolata Lukosi ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.

Mrembo huyo alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa Vodacom Miss Tanzania kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador. Mashindano hayo ya urembo yanaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2011

    Kudadeki watoto bongo wapo jamani,wacha wataalam waliotoka H-Town,TX watuambie maana washaingia mjini.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2011

    Kwani huyu Lundenga na mambo ya Umiss mpakalini??.Ndio maana ushindi haupatikani kwani kuwaharibu hao mabinti ndio swala zima.Kila siku Umiss na Hashimu Lundenga sio akili hata kiduchu nahisi siku akipotea lundenga hapa ndio Tanzania itashinda umiss kwani huwezi peleka bindiyako kwaajili ya mambo ya kutendwa.-Dako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...