Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dr Paul Msemwa akimkaribisha Balozi wa China nchini Mh LIU Xinsheng

Balozi wa China Mh LIU Xinsheng na Mkurugenzi wa Nyumba ya Utamaduni Dr Paul Msemwa wakisaini fomu za makabidhiano ya Runinga.

Dr Paul Msemwa akimkaribisha Balozi wa China Mh LIU Xinsheng nchini (kulia) pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi huo.

Balozi wa China nchini Mh LIU Xinsheng akiwa kwenye banda linalo onesha mchango wa nchi za nje ikiwemo china katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa China na Familia zao wakiwa katika onesho la Urithi wa Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika. Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar.

NA SIXMUND BEGASHE.

Watanzania wametakiwa kuheshimu na kuulinda Uhuru wa nchi hii ambao ulipatikana kwa tabu chini ya muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Jamuhuri ya watu wa China hapa nchini Bwana LIU XINSHENG alipo tembelea onesho maalumu la URITHI WA HARAKATI ZA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA linalo endelea katika kumbi za MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UTAMADUNI Dar es Salaam.

Mheshimiwa Balozi wa China nchini amesema kuwa ofisi yake imeona ni vyema ikawatembeza wafanyakazi wote wa ubalozi huo na familia zao Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ili kupitia onesho hili maalum watu Wachina wajifunze, Ushirikiano ulio dumu muda mrefu na Mchango wa nchi hizi mbili katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.

Balozi wa China aliongeza kuwa vijana wa China wajifunze ukaribu wa nchi yao na Tanzania katika kuimarisha undugu, upendo na mashikamano ulioanza tangu miaka ya sitini.

Pamoja na Matembezi hayo Balozi wa China nchini ameipatia Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Runinga yenye ukubwa wa inchi 29, ili kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni katika kurithisha elimu kwa jamii hasa vijana juu ya thamani kubwa ya amani, upendo na mshikamano wa kitaifa uliotokana na historia ya Nchi hizi mbili.

Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni – Dar es Salaam Dr Paul Msemwa aliushukuru Ubalozi wa China kwa mchango mkubwa ulio toa kwani utasaisia zaidi harakati za utoaji elimu kwa jamii hasa vijana wa nchi hii ambao ndio nguzo ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...