Ndugu Watanzania  wote waishio New York na maeneo ya karibu na pia yeyote yule
anayeweza kufika kutoka popote pale alipo. 

Ninapenda kuwatangazia kuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mh. Dr. Mohammed Gharib Bilal atakutana na WatanzaniaJumapili hii, June 12, 2011. Mkutano huu utafanyika nyumbani kwa Balozi waTanzania Umoja wa Mataifa, Mount Vernon New York saa nane kamili mchana. 

Anwani utakapofanyikia mkutano huu ni:
30 Overhill Road, Mount Vernon NY 10552.

Mnaombwa wote kuhudhuria kwa wingi ili tuweze kumsikiliza kiongozi wetu na vilevile kutoa maoni kuhusu shughuli za maendeleo na ujenzi wa taifa letu hukonyumbani. Tafadhali tujitahidi kufika mapema.

Ahsanteni,
Vincent Mughwai
Katibu
New York Tanzanian Community


New York Tanzanian Community inawakaribisha kwenye website
yetu www.nytanzaniancoomunity.org kwa habari zaidi kuhusu jumuiya yetu. Pia
tunapenda kumkaribisha Mtanzania yeyote aishiye maeneo ya New York, Connecticut,
New Jersey na Pennsylvania kuwa mwanachama wa jumuiya yetu lakini hata ndugu
zetu waishio maeneo mengine hapa Marekani wanaweza pia kuwa wanachama. 



Nia yetu ni kuhamasisha umoja na ushirikiano miongoni mwetu ili kuweza (kwa pamoja) kutatua matatizo yetu ya kijamii na kiuchumi hapa tuliko na pia kushiriki
kikamilifu katika shughuli za uwekezaji na ujenzi wa taifa kwa ujumla huko
nyumbani.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2011

    WATANZANA? jamani kazi ipo kweli kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...