Kamati ya mashindano ya ngoma ya Balimi Extra Lager kutoka kushoto ni Afisa utamaduni kanda ya ziwa Mufungo P. Mufungo, Afisa utamaduni Mwanza Makenke, meneja masoko kanda ya ziwa (TBL) Andrew Mbwambo, Special Event Erick Mwayela na majaji kutoka Butimba.
Erick Mwayela akimpongeza Godifrey Majula baada ya kikundi chao cha Utandanazi Cultural kutoka Ukerewe kuchukua ubingwa akipokea Tshs 500,000/=, mshindi wa pili ni kikundi cha Mang’ombega Kijiji kutoka Misungwi ambao walishinda Tshs 400,000/=, wa tatu ni Angano Cultural Group kutoka Ilemela Mwanza waliopokea kitita cha Tshs 300,000/=. Nafasi ya nne ilikamatwa na Chapakazi kutoka Nyamagana Mwanza na nafasi ya tano ni Makumbusho kutoka misungwi.
Mwanalyaku Group kutoka Magu wakati wa mashindano haya yaliyofanyikia viwanja vya CCM Kirumba tarehe 18/6/2011.
Utandanazi Group kutoka Ukerewe wakionyesha umahiri wao wa kusakata ngoma wakati wa mashindano hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...