ANKAL MICHUZI

LEO NIMEKUTANA NA MKASA WA KITAPELI AMBAPO ASUBUHI NIKIWA NJIANI KUELEKEA KAZINI NIKAPIGIWA SIMU NA MTU ALIEONEKANA KUTAJA JINA LANGU KWA UFASAHA, AKIDAI KUWA ANANIFAHAMU NA KWAMBA YEYE KWA SASA YUPO NJE YA DSM AKIOMBA NIMSAIDIE NIWAPIGIE PARTNERS WAKE WA KIBIASHARA KUSUDI KUJUA KUWA DAWA HIYO WANAYOIUZA INAUZWA KIASI GANI KWENYE SOKO.

UJUMBE WA SIMU ULIOTUMWA KWANGU BAADA YA MAONGOEZI NI HUU "DAWA INAITWA DAMOLINE LIQUID BEST IN FOOD 1000MLS 68F MADE IN SWEEDEN, KUNA MTU ANAITWA DR PETER PAIR 50'

KILICHONIFANYA MWANZONI NIMSIKILIZE NI KUTAJA WATU NINANAOWAFAHAMU KWA UFASAHA ILA BAADAE ALIOPOONYESHA KUWA KAZI NINAYOFANYA NINAWEZA KUIACHA KWA MUDA KWANI MIE SITAKI PESA.

HUYO "DR PETER" ANA SIMU IKO MTANDAO WA TIGO, NA HUYO ALIEKUWA AKIPIGA MWANZONI YUKO NA NUMBER YA VODACOM,

BAADA YA KUSHTUKIA NIKAWAAMBIA HUYO MTU NINAYEMFAHAMU WAMWAMBIE ANIPIGIE NITAWASAIDIA, NDIO WAKAINGIA PORINI HADI SASA.

NAOMBA NISAIDIE KUWATUMIA WADAU.....
MDAU ALIEPONEA CHUPUCHUPU KULIZWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    Asante mdau na pole sana kwa kupona..Kuna mdau mmoja alilizwa mwaka 2008 au 2009 sikumbuki vizuri mwaka na akapost humu huu mchezo.Nilisoma humu kwenye BLOG YETU KONGWE.Michuzi kama bado unacho hicho kisa waweza kukibandika tena.Nakumbuka yeye alienda hadi Airport kusubiria ndege iliyokuwa inatoka KIGOMA na huo "ujumbe mzito wa WFP"baada ya kuwa amefanyiwa uhuni huo.Pale airport akaambiwa hakuna ndege ya aina hiyo kwenye ratiba yao ya siku hiyo na akaambiwa yeye alikuwa kama mtu wa 6 hivi kuripoti hapo Uwanjani.!!!Ningekuwa mimi ningewalengesha kwenye mtego wa police manake nilikuwa aware na huo mchezo..bahati yao.

    SIMU ZA MIKONONI:Hizo namba ulizopewa zimesajiliwa au ???..au zilikuwa 'disposable'?coz these guys are very very clever.

    Mdau.David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Kuna watu wanauza sabuni za kusafishia choo. Huchukua sabuni za bei ndogo, wakaziyayusha na maji wakaweka rangi na mafuta mazuri. Wanauza gallon Tsh3000. Hutembeza mitaani.

    Kuna wengine wanauza asali. Huchukua asali kidogo wakaweka kwenye chupa baadae wakajaza shira (sukari iliyochemshwa na maji). Wanauza lita Tsh5000.

    Wengine wanauza mchele wa Mbeya, wanaweka mawe na michanga chini tele. Gunia la kilo mia, mchele ni kilo hamsini. Gunia Tsh 90,000.

    Wauza mkaa nao ukinunua gunia moja, chini wanaweka chenga tupu. Robo tu ndio mkaa. Gunia Tsh5000.

    Wangekuwa wanasiasa tungewaita mafisadi, je hawa tuwaite nani?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2011

    ..."Wauza mkaa nao ukinunua gunia moja, chini wanaweka chenga tupu. Robo tu ndio mkaa.
    Gunia Tsh5000"...

    Kuhusu wauza mikaa, nilikuanikiwaambia tunamwaga kwanza tuone chini walikua wanakataa biashara!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2011

    Fisadi ni fisadi tu. Na huu ufisadi unawaona wengi ambao ni watoto wa hao mafisadi ndio unaona vijana wadogo wanatembea na Land Cruiser VX wenyewe wakienda krismas huanza hustaajibiana eh wewe umetoka hapa hohe hahe umeshakuwa hivi, hongera sana bwana. Takriban watanzania wengi ni mafisadi, hata hao wanaowataja wenzao ni mafisadi na wao vile vile. Zamani wafanyakazi wengi wa serikali na mashirika ya umma walikuwa wakifuga kuku na ngombe, kumbe ni geresha tu huku anachota kwenye shirika analofanya kazi. na mpaka leo mchezo huu unaendelea, halafu kanunua prado vx. Sasa watu utawasaidia eh! mradi wako wa kuku umekuletea mafanikio kweli. Hivi kweli mradi wa kuku ulipie watoto shule tena ulaya, ujenge jumba la fahari, uwe na mashamba na ununue magari. kama sio ufisadi ni nini. Acheni kutudanganya sisi walala hoi. Akine Mbowe, Slaa wametoka wapi si ndo hao hao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2011

    Hata mm yalinkuta jana tena anasauti ya kichanga ili nilimshtukia kwa sababu hakuwa na maelezo kamili kuna sehemu alijichanganya kidogo nikamsikiliza nikamwambia unajua kuna Matapeli mwambie Boss wako anikol basi mara akasema ooh ngoja nipokee simu ...Kadai yuko Ngara kawa Dereva huko Un ila kwa sasa unajua huko hamna wakimbizi wako walemavu tuu na wazee sasa niwasaidia namba ya huyo TAPELI NI 065404093 lifanyieni kazi wajinga anaongelea about million 30 nilipomwambia kuna wezi na matapeli toka jana kimnyaaaaaaaa kaona nilimstukia

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2011

    MADUKANI na MABUCHANI: MZANI wa kupimia hauna kitu ila jiwe la kupimia uzito limeshawekwa ili tuuziwe NUSU na ROBO badala ya KILO MOJA.

    wote ni wahujumu uchumi na inabidi ifike kipindi watanzania tuseme hapana na hawa watu tuwashughulikie ipasavyo pindi tu wanapogundulika.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2011

    Cha msingi ni kuacha tamaa tu ya utajiri wa haraka haraka ndio hawa jamaa utawezana nao. Mimi mwenyewe walishawahi nipigia simu nikiwa pale mahakama ya rufaa,tena wakawa wanataja kila detail yangu,cheo changu na kazi nayofanya wanaomba niwasaidie wazungu wao wamefikia hapo kempinski,mie nimpigie huyo dr.wao anipe sample ya hiyo dawa nikawaoneshe hao wazungu,na baadaye hao wazungu wakinipigia niseme hiyo dawa ninayo pc 50 na naweza kuwasupply kwa dola 2500,katika hizo hao jamaa wa kigoma wakasema likifanikiwa tutagawana ile dola 500 ya juu kwa kila pakiti. Mie nikawa nimewatega tu na kuwasikiliza na kufanya kila wanachotaka. Sasa mwishoni wale wazungu wakadai niende na sample,jamaa wa kigoma wakadai nimshawishi dr,anipe,dr akasema hanipi mpaka japo nipeleke dola 2500 ya paketi moja,naye muda huo anaelekea mitaa ya KAIRUKI kupeleka nyingine kwa wateja. Hapo nikamwambia jamaa wa kigoma siwezi kufanya hizo deal kwakuwa sina hiyo dila 2500 labda yeye anirushie kwa M-PESA nikamnunulie. BASI tukashindana kwa terms hizo.Kwa ufupi ilinisaidia kwakuwa nilikuwa najua ni matapeli ila nilitaka kuconfirm tu and thanks kwa MICHUZI Blog kwa kuwa niliwahi kuwasoma hawa jamaa hapa.
    Ila wana mbinu kali sana,na hizo namba wanazo nyingi na wanabadili kila leo,na huyo mzungu hata sio mzungu kuna namna ya kubana pua kuweza kuongea kama hivyo. Wameshawaliza watu wengi sana,tena wasomi na wanasheria wakiwemo. POLISI washaripotiwa hili sana.
    Poleni sana mliolizwa but we must be careful

    ReplyDelete
  8. namba zao hizi hapa...0652 - 799781, 0752 - 548626, 0718 - 392114, 0714 - 302068

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...