Beki wa Yanga aliyesajiliwa msimu huu akitokea timu ya JKT Ruvu, Oscar Joshua (kushoto) wakati wa mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu pamoja na michuano ya kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mashabiki kibao uwanja wakiangalia 'vifaa' uwanja wa Kaunda asubuhi hii
 Wana Yanga wakiangalia 'vifaa' uwanjani
 Tizi golini
 Kati ya uwanja
 Tizi la kukimbia
Kipa aliyesajiliwa kutoka Majimaji ya Songea, Said Mohamed akiwa katika mazoezi ya timu ya Yanga kwenye Uwanja wa Karunda jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2011

    Wafadhili na viongozi wawalipe wale waliopo pale bondeni ili wahame nasi tujenge uwanja wa kufa mtu pale na kuongeza mapato ya CLUB

    ReplyDelete
  2. ha ha ha! hizo ndizo habari zinazotakiwa. nawapa hongera sana Uongozi kwa maandalizi. kila la kheri.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2011

    Dah, Yanga timu yangu lakini uwanja nomaaa....umechakaa kiasi cha kutisha....huwezi kuamini hata hao wachezaji wanafanya mazoezi hawaumii...babu nomaaa...Jamani tutabadilika lini, kila kukicha ugomvi kwenye vilabu,dhiki zimetujaa kwa pesa....kuanzia Timu ya Taifa mpaka Vilabu utumbo mtupu...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2011

    ngangali kweli kweli!! gangamala mwanangu!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2011

    ukisikia uvivu ndio huu.. yani watu wamejazana mazoezini asubuhi yote badala ya kutafuta shughuli za kujiongezea kipato??? mara mia wangekuja jioni lakini asubuhi????
    bongo kweli tambarare..

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 16, 2011

    hivi hii timu haina jezi za mazoezi,kila mtu na nguo zake,MNATIA AIBU YANGA,BADILIKENI na sio lazima mfanyie mazoezi kwenye kiwanja kibaya

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 16, 2011

    Ningekuwa na kiboko, ningewatandika viboko hao mashabiki wa Yanga wanaoenda kuangalia mazoezi asubuhi asubuhi badala ya kwenda kazini!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 16, 2011

    Jamani na mie nalia kiwanja kibovu kwa timu kama Yanga, ingawa si mshabiki wa Yanga, kiwanja jamani. Timu kama Simba na Yanga zimekaa miaka mingi mno kutokuwa na kiwanja chao kizuri, tena cha nyasi, ni kutunza tu. Nazijua timu dalaja la tatu huku Mbeya wana viwanja bora.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 16, 2011

    Harama za kupanda majani ni Tsh400,000@12 mshahara, Tsh10,000,000/= vifaa na majani kwa mwaka. Je Yanga watashindwa na Tsh15,000,000/= kila mwaka kugharamia majani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...