Beki wa Yanga aliyesajiliwa msimu huu akitokea timu ya JKT Ruvu, Oscar Joshua (kushoto) wakati wa mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu pamoja na michuano ya kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mashabiki kibao uwanja wakiangalia 'vifaa' uwanja wa Kaunda asubuhi hii
Wana Yanga wakiangalia 'vifaa' uwanjani
Tizi golini
Kati ya uwanja
Tizi la kukimbia
Kipa aliyesajiliwa kutoka Majimaji ya Songea, Said Mohamed akiwa katika mazoezi ya timu ya Yanga kwenye Uwanja wa Karunda jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii









Wafadhili na viongozi wawalipe wale waliopo pale bondeni ili wahame nasi tujenge uwanja wa kufa mtu pale na kuongeza mapato ya CLUB
ReplyDeleteha ha ha! hizo ndizo habari zinazotakiwa. nawapa hongera sana Uongozi kwa maandalizi. kila la kheri.
ReplyDeleteDah, Yanga timu yangu lakini uwanja nomaaa....umechakaa kiasi cha kutisha....huwezi kuamini hata hao wachezaji wanafanya mazoezi hawaumii...babu nomaaa...Jamani tutabadilika lini, kila kukicha ugomvi kwenye vilabu,dhiki zimetujaa kwa pesa....kuanzia Timu ya Taifa mpaka Vilabu utumbo mtupu...
ReplyDeletengangali kweli kweli!! gangamala mwanangu!!!
ReplyDeleteukisikia uvivu ndio huu.. yani watu wamejazana mazoezini asubuhi yote badala ya kutafuta shughuli za kujiongezea kipato??? mara mia wangekuja jioni lakini asubuhi????
ReplyDeletebongo kweli tambarare..
hivi hii timu haina jezi za mazoezi,kila mtu na nguo zake,MNATIA AIBU YANGA,BADILIKENI na sio lazima mfanyie mazoezi kwenye kiwanja kibaya
ReplyDeleteNingekuwa na kiboko, ningewatandika viboko hao mashabiki wa Yanga wanaoenda kuangalia mazoezi asubuhi asubuhi badala ya kwenda kazini!
ReplyDeleteJamani na mie nalia kiwanja kibovu kwa timu kama Yanga, ingawa si mshabiki wa Yanga, kiwanja jamani. Timu kama Simba na Yanga zimekaa miaka mingi mno kutokuwa na kiwanja chao kizuri, tena cha nyasi, ni kutunza tu. Nazijua timu dalaja la tatu huku Mbeya wana viwanja bora.
ReplyDeleteHarama za kupanda majani ni Tsh400,000@12 mshahara, Tsh10,000,000/= vifaa na majani kwa mwaka. Je Yanga watashindwa na Tsh15,000,000/= kila mwaka kugharamia majani?
ReplyDelete