MECHI KATI YA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA NA AFRIKA YA KATI INAENDELEA KUCHEZWA HIVI SASA HUKO NCHINI AFRIKA YA KATI NA HIVI SASA NI KIPINDI CHA PILI CHA MCHEZO HUKU TIMU YETU YA TAIFA IKIWA NYUMA KWA BAO MOJA LILILOFUNGWA MNAMO DAKIKA YA 37 YA MCHEZO KUTOKANA NA MAKOSA KIDOGO YA MABEKI WETU.

KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA LEO KIKO NA WACHEZAJI,SHAABAN KADO,SHADRACK NSAJIGWA,IDRISA RAJAB,HENRY MORRIS,NADIR HAROUB,NDITI,JUMA KAZIMOTO,NUDRIN BAKARI,JOHN BOCCO,NIZAR KHALFAN PAMOJA NA MRISHO NGASSA.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA TOKA KWA RIPOTA WETU ALIEONGOZANA MA TIMU YA TAIFA HUKO AFRIKA YA KATI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    Tumechabangwa 2-1. Ni kosa la Maximo? Sasa hivi timu yetu inaenda uwanjani tunaogopa kupigwa. Enzi za Maximo tulikuwa hatumwogopi mtu. Bora hata hiyo timu tungempa Julio!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2011

    Julio bonge ya kocha...kawatoa Wacameroon na sasa Nigeria wameshaanza kuona moto wake..peana timu wazawa alafu muwalipe kama hao wazungu kama hatutaendelea!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2011

    Hakuna cha wazawa wala nini! Wazawa wana Usimba na Uyanga sana. Hata huyu mzungu wameshamharibu ni Simba wazi kabisa kumuita Machupa na kumuache Tegete si uwendawazimu huo.
    Kwanza naona wachezaji wanaingizwa timu ya taifa KIUDINI. Lazima tuseme! wachezaji ngangali wapo kibao huku kanda ya ziwa pia Mbeya lakini wanaitwa watu akiwekewa panja tu anaanguka mwenyewe toka utotoni analalia chai na chapati moja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...