Home
Unlabelled
mh zitto kabwe aendelea kupiga vita posho za vikao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hi safi
ReplyDeleteRafiki yangu Zitto. Nia yako ni nzuri kwa maendeleo ya nchi. Lakini katika viongozi wenzako upo peke yako mwenye moyo kama huo. Kwa sababu hiyo, wazo lako halitakubaliwa hata siku moja. Ungeendelea tu kukinga posho yako bila hata kuitoa sadaka kwa tasisi. Labda kama hiyo taasisi ni ya kwako.
ReplyDeleteKitu cha msingi Zitto, mngeendelea tu kuibana siri-kali ili idhibiti matumizi ya pesa kwenye tasisi na idara zake ili waelekeze pesa hizo kwenye maendeleo ya nchi hasa kwa watu wa chini. Lakini kukataa posho sio suluhisho kwa vile zitaendelea kubaki hazina na zitaliwa na wajana wengine.
ReplyDeletePosho za vikao sinasaidia wafanyakazi kuongeza kipato chao. Hii hufanya mabosi wajipeleke vikao, semina na warsha zote wao pekee na marafiki zao. Kuondoa hii ni jambo zuri. Isipokuwa sasa itabidi serikali iongeze mishahara ili wafanyakazi wasifanya shughuli zengine wakati wa kazi.
ReplyDeletewajitokeze na wengine pleaseee! hongera zito na asante!
ReplyDeleteAsante Zitto kwa moyo wa Kizalendo uliouonyesha. Lakini kwangu mimi hapo hujaacha kuchukua posho na stahili zako isipokuwa ulichokifanya ni kuzipangia matumizi mengine tofauti na ya awali. Ulichokifanya hakina utofauti na allwance za jimbo tunazozisikia au kwa mwingine kutumia hela hizo kulipia watoto yatima karo n.k.katika jimbo lake. kwani tazama umeagiza pesa zote zipelekwe Kigoma (KDI)! Kwa ushauri wangu either ungezikataa zirudi hazina zikapangiwe matumizi mengine kwa manufaa ya Watanzania wote hata mimi kalagabaho zinaweza kunisaidia. Au ungezitoa kwa wahitaji kama yatima, walemavu wa ngozi n.k. kutoka maeneo yote bila kuzingatia unakotoka, hii ingetujengea imani kweli ulidhamilia. Lakini jinsi hii ilivyokaa, kwangu ni danganya toto!
ReplyDeleteMh Kabwe, kwa heshima ndugu yangu
ReplyDeletepia nakuomba upige vita hiyo "posho" ya slaa ya shilingi milioni saba (!!!!!) kwa mwezi ambayo, kama alivyosema mbowe, imeitwa "posho" badala ya mshahara ili isilipiwe kodi ya mapato. Vinginevyo hiyo hoja yako itaonekana kuwa ni hatua nyingine ya chadema ya danganya toto tu.
Mimi ni mwanachama wa CCM. Nakubaliana na Mhe K Zitto kuwa hiyo sitting allowance ifutwe tu kwa kuwa tayari wabunge wakiwa kwenye session ya bunge wanalipwa masurufu ya kujikimu (per diem, n.k.). Nawasilisha rasmi.
ReplyDeleteNi sawa kabisa. Ila pia tunaomba kuwa wabunge wa Chadema pia waache kupewa posho na chama hicho kila waendapo bungeni. Kwa sasa, wabunge wa Chadema wanapewa posho ya serikali na posho ya chama chao. Hii pia itasawazisha uwanja wa maslahi.
ReplyDeleteSasa wewe unayesema Slaa anyang'anywe posho yake wakati wabunge wote wanalipwa milioni 7.1? Utakuwa hujamtendea haki kusema yeye alipwe tofauti na wenzake.
ReplyDeleteMimi ningewashauri kitu kimoja. Kama wazo la kukatwa posho litapitishwa, mngelenga kutatua tatizo moja baada ya jingine kwa kutumia posho hizo. Kwa mfano, Dar kuna foleni kubwa ambayo inasababisha taifa linapoteza mabilioni ya pesa kwa watu kuchelewa kufika kazini au mahali wanapotakiwa kuwepo. Na pia wawekezaji wengine wakifikiria foleni huamua kuahirisha kuwekeza Tz. Kwa hiyo mngesema posho ya kikao cha mwezi fulani na fulani zikatwe ziende moja kwa moja kujenga barabara za juu kwenye makutano ya barabara. Mkifanya hivyo mtakuta mmetatua matatizo sugu ambayo yangechukua karne nyingi kutatuliwa. Lakini mkisema posho zirudi hazina, hakutakuwa na tofauti yoyote kwani zitapangiwa matumizi mengina ambapo mwishowe zitaendelea kuishia mikononi mwa akina fisadis.
ReplyDeletemie angesema hataki kabisa ningemuona wa maana wa sana! lakini hata hivyo a way forward!
ReplyDeleteNi jambo zuri na la busara kwa maendeleo yetu.Nadhani mheshimiwa ungeendelea kuibana serikali ili iwe ni zoezi la wabunge wote kwa ujumla.
ReplyDeletePili,hapa kidogo pia pana nia binafsi...Je kulikuwa na haja ya ku-post barua hii kwa michuzi !!! Mi nadhani msisitizo wako upeleke bungeni na pindi wananchi wahitajipo kujua michango waweze kuitisha kumbukumbu za vitabu vya bunge....hata hivyo nakupongeza kwa jambo uloliamua. Asante
kuna mapungufu ya kimfumo kwetu afrika.mimi nilipokuwa bongo nilikuwa nikienda training yoyote nadai allowance kwa nguvu zote.nilipoingia ulaya jamaa hawa wakikutuma training wanabajeti iendane na muda wa kazi malipo yale yale.Sisi bado ni masikini sana na ili tuendelee tunahitaji mhanga wa hali ya juu.zito angalau amejaribu hata kuthububu kuwa na hatua,iwe kwa manufaa ya chadema au binafsi. hebu angalieni comment hata anaetegemea kufaidika na hiyo pesa anamuona kama zito hana akili.Huo ndio utanzania hakuna alie na machungu sidhani kama tutatoka.Eee mungu tusaidie
ReplyDeleteMheshimiwa Zitto hongera sana kwa uamuzi huo wenye maslahi kwa taifa na kwa wananchi wako wa Kigoma. Mimi nimekuelewa kabisa na kama wengine (wabunge) watakuunga mkono basi, maendeleo walau wataanza kuonekana. Uamuzi wa kupeleka posho hiyo katika mfuko wa maendeleo ya Kigoma ni bora kabisa kuliko kuruhusu wapeleke hazina. Wewe kama mbunge wa Kigoma unastahili kuamua hivyo. Naamini uamuzi huu utazidi kukujenga na kukufanya uzidi kukubarika. Hongera sana.
ReplyDeleteHao wanaojifanya vichwa ngumu waambieni wabunge wenu nao wapeleke kwenye majimbo yao ili pesa hizo zisaidie kuleta maendeleo kwenu. Huu ndo utakua mfano wa kujua wabunge wenu hawakwenda kuwatetea bali kujilimbikizia pesa wakati wanajua kabisa baada ya miaka mitano wanapewa milioni zaidi ya 50 kama malipo ya pensheni, wakati wewe ukifanya kazi miaka kumi, utaishi kwa shida na kamshahara kako kadogo hata pensheni ya milioni 5 hupati. Mnaonewa huruma na vijana wenye nia njema na nchi wanao pambana kuondoa siasa za kudidimiza maendeleo ya taifa mnapinga kelele. Tunahitaji Vijana wazalendo kama Zitto msikalie kudanganywa na wanasiasa walaku eti vijana ni taifa la kesho,hiyo kesho imeshafika. Vijana mtanatakiwa kutetea masilahi yenye manufaa kwa wananchi na sio ya mwananchi mmoja mmoja. Waambieni wazee wanayoyafanya si misingi mizuru kwa vijana wanaodaiwa kuwa taifa la kesho. Kwanza vijana wengi wapo vijiweni nafasi zenu zimezibwa na wazee amabao wana mambo mengi kichwani ndo maana hawawezi acha kuchapa usingizi bungeni akitoka ana laki na nusu bado hajapiga mahesabu ya miradi yake na mshahara unamsubiri. Ukweli ni kwamba akipokea hiyo laki na nusu kwa siku kumi na tano ni sawa na mshahara wa mfanyakazi wa serikali kwa muda wa mwaka mzima. Sasa nyie watu hata hamshituki hata kujionea huruma ama wamewalonga ama mnakubali kuchinjwa kama kondoooo.
ReplyDeleteHONGERA SANA BWANA ZITTO KABWE. MTU MMOJA KASEMA KWAMBA MHESHIMIWA ZITTO KUPELEKA FEDHA HIZO KWENYE FOUNDATION HUKO KIGOMA NI SAWA NA KUICHUKUA POSHO MWENYEWE, SI KWELI. FOUNDATION ANAYOIPELEKEA HELA ZITTO NI UMMA WA WANANCHI WA TANZANIA AMBAO SI MBUNGE ANAYEKULA HIZO FEDHA. ZITTO ANA NDUGU ZAKE WAJOMBA NA SHANGAZI, NA WADOGO ZAKE PIA, ANGEWEZA KUZIPELEKA HIZO HELA FAMILIA YAKE IFAIDI. LAKINI KWA KUTAMBUA KUWA HIZO HELA ZINATAKIWA KULETA AUHENI YA WATANZANIA KAMA JAMII, NDIO MAANA KAPELEKA HUKO. HUU MFANO UNAPASWA KUIGWA NA WABUNGE WOTE, AMBAO WAMEKWENDA BUNGENI KWA LENGO HASWA LA KUIKOMBOA TZNZANIA. MIMI NIPO NJE YA TANZANIA NA NILISHAKUWA MTUMISHI SERIKALINI TANZANIA. KILA NILIPOFANYA KAZI NJE YA KITUO KWA SIKU CHACHE TU, NILILIPWA HELA NYINGI KULIKO MSHAHARA WA MWEZI MMOJA. NIKIWA HUKU, BADO NAFANYA KAZI NJE YA KITUO AU SAA ZA KAZI. NINACHOLIPWA KWAKWELI SI NYINGI KIASI NILICHOKIONA TANZANIA - NCHI MASKINI! HAPA NARUDISHIWA NAULI TU NIKISAFIRI, AU KAMA KUNA KIKAO, NITAPEWA CHAKULA CHA BURE NA TUTALIPIWA SI KUPEWA HELA TASLIMU. ANAYEPINGA WAZO LA ZITTO KABWE HAWATAKII MEMA WATANZANIA WOTE. WATANZANIA MSISAHAU, ZITTO PIA ALISHAWAHI KUTOA MFANO KWA KUREJESHA MKOPO WAKE ALIOPEWA ILI ASOME CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM. WANGAPI NI VIONGOZI WA TANZANIA WAMEKAUSHA?????
ReplyDeleteELIMU TUNAYOIPATA WALAI HAITUKOMBOI. INATUANDAA SISI WATANZANIA KUWA TABAKA LA MKOLONI WA RANGI NYEUSI. HAKUNA TOFAUTI NA MZUNGU ALIYETUTAWALA ZAMANI. TUMEBADILI TU NGOZI.
jamani mnajua mishaara ya serikali ama Zitto anaongea tuu? angesema posho zifuntwe na mishaara iwekwe sawa..kwani mshaara wa graduate ni laki 280 sasa ataweza ishi vipi na maisha ya sasa?
ReplyDeleteCHANGA LA MACHO, TOA MFUKO HUU WEKA MFUKO ULE.
ReplyDeleteKUKATAA MAANA YAKE NI KUSUSA, SASA HAPA AMEELEKEZA POSHO ZAKE ZIPELEKWE MAHALA FULANI TU, HAKUNA JIPYA BADO ANAZICHUKUA.
ZITTO ANATAFUTA URAIS BAADAE KWAHIYO AKAANZA NAMNA HII WATU BAADAE WATAMCHAGUA! KUTAFUTA KURA ZA WANANCHI LAZIMA UANZIE KIGOGO KIDOGO NAMNA HII. MWENZENU MJANJA HUYU!
ReplyDeletePosho hiyo usiielekeze jimboni mwako tu na walalahoi sie wengine wengine tuifaidi pia muheshimiwa
ReplyDeletezito kama kweli ana nia ya dhati kwanini asipeleke hoja bungeni ijadiliwe ...huwezi kubadili sheria kwa kumuandikia spika barua...huku ndio kutafuta umaarufu......walimu.polisi madaktari na wataalamu wengine ndio wangestahili kulipwa milioni 7 ila sio kwa tanzania hii tuijuayo....zito fuata njia sahihi za kuwasilisha hoja tuone kama kweli una nia ya dhati..maana mpaka sasa mimi na wenzangu wengi tumepoteza imani na chama chako kwani hoja zake nyingi ni za kutafuta umaarufu na hazina manufaa zaidi ya kusababisha vurugu na maandamano
ReplyDeletewakatabahu