Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi (wa nne shoto) akiwa meza kuu na viongozi wengine wakishuhudia mechi ya ufunguzi ya michuano ya Copa Coca Cola jioni jana uwanaja wa Karme jijjini Dar kati ya Dodoma na Kinondoni
Si uchezaji tu, siku hizi vijana wanajifunza kuwa waamuzi wa soka ambapo pichani ni baadhi ya vijana 20 wanaosomea urefa katika kituo cha michezo cha Abdallah Twalipo jijini Dar ambao ndio wanaochezesha katika michuano ya mwaka huu ya Copa Coca Cola

 Walezi wa timu za vijana toka nchi nzima zinazoshiriki Copa Coca Cola 2011
 ITV na Radio One Stereo wanaonesha michuano hiyo na kuitangaza live. Hapa Maulid Baraka wa Kitenge akiongoza kikosi kazi cha utangazaji huo wakati wa mechi ya ufunguzi
 Mpiganaji Jamal Rwambow (kulia) akiwa na MC wa shughuli hii Ephraim Kibonde (shoto) na mdau  
Sehemu ya uwanja wa Karume wakati wa mchezo wa ufunguzi
Mkurugenzi mtendaji na mtangazaji wa Sport FM Abdallah Majura akiwa kazini kwenye ufunguzi wa michuano hii

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi, amezindua rasmi msimu wa Tano wa michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ulioanza jana  katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika viwanja vinne tofauti.Uzinduzi  huo umefanyika Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam.


Mikoa yote 28 ya Tanzania Bara na Visiwani inashiriki katika michuano ya mwaka huu. kila siku kutakuwa na mechi mbili kwenyeviwanja vyote. Mechi ya kwanza itaanza saa 2.30 asubuhi wakati ya pili itachezwasaa 10 jioni.
Mechi maalumu ya uzinduzi ilikuwa  kati ya bingwa mtetezi Kinondoni na Dodoma. Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Tamco na Nyumbu vya Mkoa wa Pwani, na Karume na Tanganyika Packers (Kawe) vya Mkoa wa Dares Salaam. 
Jana pia kulikuwa na  mechi zingine za uzinduzi kati ya Temeke na Ilala katika  Uwanja wa Tanganyika Packers, Kigoma imemenyana na  Pwani kwenyeUwanja wa Nyumbu wakati Mjini Magharibi ilicheza na  Morogoro katika Uwanja wa Tamco, Kibaha  saa 2.30 asubuhi. 

Fainali itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati waamuzi 20 ambao wana umri chini ya miaka 17 wakiwemo wasichana wawili ndiyo watakaochezesha michuano hiyo.
Hatua ya awali inachezwa katika makundi manne ya timu saba saba ambapo nne zakwanza katika kila kundi ndizo zitakazoingia hatua ya 16 bora. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...