Ndugu wapendwa,
Natumaini wote mu wazima wa hali, na shughuli mnaziendesha ipasavyo. 
Napenda kuwafahamisha rasmi kwa niaba ya wanakamati wenzangu kwamba Jumuia ya watanzania waishio New England (MA,NH,CT,RI,ME,VT na NJ), ikiwa chini ya mwamvuli wa NEW ENGLAND UMOJA FOUNDATION, INC, inawakaribisha rasmi kwenye ile shughuli ya kuvunja na shoka inayofanyika kila mwaka pale camp Keewanee, Greenfield, Ma.

Siku ya ijumaa na Jumamosi usiku kutakuwa na viburudisho rasmi kutoka kwa Ma-D.j's wetu ikiwa ni pamoja ni DJ Richimaka ambae atakuwa na vibao vipya kabisa kutoka BONGOLAND!!.

Siku ya Jumapili  July 03/2011  ndio  Shughuli yenyewe. N.E.Umoja inatimiza miaka 10 tangu zilipoanza sherehe hizi. Njoo wewe, na wale wote uwapendao ufurahi na watanzania wenzako kutoka sehemu mbalimbali, kuadhimisha siku hii muhimu tukikumbuka na kuuenzi utamaduni, desturi na mila za Ki-Tanzania!.

Shughuli hii itafanyika palepale Camp kee-wanee 
(www.campkeewanee.org), 
Greenfield MA. 01301.
(9AM-9PM).

**ILANI: POMBE NI MARUFKU KATIKA CAMP SITE...PERIOD!!!!**(THE CAMP IS ALCOHOL FREE, AND WE MUST RESPECT THAT RULE PLEASE)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2011

    Party ina masharti utadhani pakti au tangazo la sigereti.... Mnawanyanyapaa wanaopenda kinywaji chao wajemeni... si mbadili ukumbi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...