Na Woinde Shizza,Arusha
mwanamitindo wa mavazi maarufu hapa nchini,Hanifa Hashi akishirikiana na hoteli ya kitalii yenye hadhi ya nyota nne Mt,Meru wamepanga kufanya onyesho kubwa la mavazi litakalofanyika mapema katikati ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Hayo yalisemwa na afisa mahusiano wa hoteli hiyo,Mariki Theron wakati wa onyesho la mavazi lililofanyika hivi karibuni na kudhaminiwa na hoteli hiyo onyesho lililolenga kusaidia kundi la jamii ya Albino waishio mkoani Arusha.
Mariki,alisema kuwa mara baada ya uongozi wa hoteli hiyo kutambua jitihada zinazofanywa na mwanamitindo Hashi katika kusaidia makundi mbalimbali yasiyojiweza ndani ya jamii kupitia mitindo wao walifarijika na kuamua kumuunga mkono mwanamitindo huyo.
Naye mwanamitindo Hashi ambaye amefanya kazi yake kwa miaka minane sasa alisema kuwa mara nyingi amekuwa akifanya maonyesho kwa lengo la kusaidia jamii huku akibainisha kuwa mbali na kusadia kundi la jamii ya Albino waishio mkoani Arusha pia amesaidia vikundi vya Maridadi na kituo cha yatima cha Moshi-Arusha kupitia fani yake.
“Lengo langu ni kusaidia makundi yasiyojiweza ndani ya jamii kwa kuwahamasisha lakini vilevile nashukuru kwani kupitia fani hii nimeweza kusaidia watoto 21 kwa kuwapatia makazi katika eneo la Makao Mapya hapa Arusha”alisema Hashi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...