Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha
Uchumi na Mipango ya Maendeleo , Omar Yussuf Mzee
  

Na Hamad Hija,MAELEZO Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza mwelekeo wa bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2011/2012 huku ikiweka mkazo katika sekta ya kilimo, kuboresha maslahi ya watumishi wa umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo , Omar Yussuf Mzee alisema kimsingi bajeti hiyo ya shilingi bilioni 613 imekidhi mahitaji muhimu.

Waziri huyo alisema kwamba kuanzia sasa kila mfanyakazi wa Serikali atalipwa mshahara kulingana na kada yake ikiwa ni njia mojawapo ya kuvutia wataalam kufanyakazi hapa nchini.

Bajeti hiyo ni ongezeko la shilingi bilioni 166 ambapo mwaka jana SMZ ilikuwa na bajeti ya shilingi bilioni 444.

Mchango wa Washirika wa Maendeleo ni bilioni 340 katika bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mwaka 2011/2012

Waziri huyo alisema vijana wengi wamekuwa wakikataa kufanya kazi za kilimo,hivyo chini ya bajeti hiyo Serikali imeweka mpango mkakati wa kuona kilimo kinakuwa kimbilio la vijana katika uzalishaji mali.

Katika mwelekeo huo wa bajeti kwa ujumla hakutakuwa na ongezeko la kodi yoyote ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.

Waziri huyo hakuweza kueleza ukuaji wa uchumi pamoja na mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa Zanzibar ambao kwa sasa kwa sehemu kubwa unategemea sekta ya utalii ikiwa sekta kiongozi na kilimo.

Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepangwa kusomwa Jumatano wiki hii ikiwa wiki moja baada ya kusomwa kwa bajeti za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zimeamua kusoma bajeti zake siku moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...