Veronica Kazimoto na Aron Msigwa –MAELEZO, Dodoma.

Tanzania imeshauriwa kutumia mbinu mbalimbali zinazotumika katika nchi ya iran ili kukabiriana na wimbi la wizi wa kazi za wasanii.

Ushauri huo umetolewa leo na Naibu waziri wa filamu na Sanaa za Maigizo wa Iran Javad Shamaqdar wakati akizungumza na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi mjini Dododma.

Naibu Waziri huyo amesema wizi wa kazi za wasanii nchini kwake kwa kiasi kikubwa umepungua kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanyika ikiwemo usambazaji wa kazi za wasanii maeneo yote ya nchi kwa wakati mmoja mara zinapotoka.

Amesema njia hii husaidia sana kupunguza wizi wa kazi za wasanii kwa kuwa mikanda ya picha za video, Dvd na ile ya mfumo wa sauti (CDs) hupatikana kwa wingi kila mahali na kwa bei nafuu ambayo hata mwananchi wa kipato cha chini anaweza kumudu kununua kazi hizo.

“Nchi yangu kwa mfano, mara kazi mpya ya msanii inapotoka wasambazaji huhakikisha “cd” zinafika karibu maeneo yote ya nchi na kwa bei nafuu kiasi kwamba mwananchi hashawishiki kununua cd za mitaani” Amebainisha Shamaqdar.

Mbinu nyingine aliyoitaja inayotumika iran ni ile ya kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa dini ambao hutumia mahubiri na mawaidha yao kwenye nyumba za ibada kukemea watu wanaonunua kazi za wasanii zisizo halisi (original).

“Viongozi wetu wanatusaidia sana kupunguza wizi wa kazi za wasanii kwa kupitia mahubiri na mawaidha yao kwa kuwasihi waumini wao kutonunua kazi zisizo halisi (feki) kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na wizi kitu ambacho ni dhambi mbele za mwenyezi mungu”.

Ameelezea njia nyingine kuwa ni kushirikiana na jeshi la polisi, mahakama na watengenezaji wa kazi za wasanii (producers) kuhakikisha wanawakamata wezi wa kazi za wasanii na kuharibu kazi walizonazo pindi wanapowakamata pamoja na kuwatoza faini.

Hata hivyo Naibu waziri huyo wa Iran amefurahishwa na hali ya amani na utulivu na mshikamano uliopo nchini Tanzania ambao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na watanzania wenyewe kuheshimiana na kutobaguana kwa misingi ya dini, kabila wala rangi na pia hali ya kuheshimu na kudumisha utamaduni uliopo.

Kwa upande wake waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emanuel Nchimbi amemshukuru kiongozi huyo na ugeni alioambata nao nchini Tanzania huku akikiri Tanzania kukumbwa na tatizo hilo la wizi wa kazi za wasanii na kuahidi kuwa wizara yake inafanya mpango wa kushirikiana na nchi ya Iran ili kubadilishana uzoefu wa kukabiliana na tatizo la wizi wa kazi za wasanii.

Aidha Dkt. Nchimbi amefafanua kuwa Tanzania inaweza kushirikiana na nchi ya Iran katika matumizi ya lugha ya Kiswahili katika tasnia ya filamu za Iran kwa kuwa inao wataalam wa kutosha wa lugha hiyo ambayo hivi sasa inatumiwa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo kukubaliwa kutumika katika mikutano ya Umoja wa Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2011

    Iran? You must be joking.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2011

    "Iran? You must be joking." My sentiments exactly!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2011

    KWANINI WAZIRI !!!ACHICHUE SISI WANANCHI WANYO KUSAIDIA HIYO KAZI

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2011

    Kwanini msitupe hito kazi sisi Watu wa Nyayo,ile cold war iliisha,every know Sasa Mt.kilimanjaro siyo Mt Kenya,Malaika song ilipigwa Tza 1950-1960 ila Fadhili William Alikua First to Record,Juma ikangaa na Fillybatbay walizaliwa Kenya wakaenda Tza kama experts wa jeshi,Pia Samahani kwa Uzembe wa kifo cha Hayati RIP mubaraka mwinyisehe.
    kazi hiyo tungeiweza sisi kwa sababu tunaifahamu Tza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...