Kituo kipya cha Daladala cha Mbezi sasa kipo katika hatua za mwisho mwisho kama picha hii inavyoonyesha,ambapo Daladala zote zitakuwa zikipaki hapa kwa kupakia na kushusha abiria na kuondoka katika kile cha zamani ambacho ni kidogo ukilinganisha na idadi ya magari yanatoingia kituoni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2011

    Nashukuru sana kwa kuleta habari hii na nilikuwa natafuta sehemu ya kuwasilisha maoni yangu juu ya kituo hiki. Kwanza nawapongeza wote waliofanikisha ujenzi wa kituo hiki.

    Tatizo langu ni kutofikiria mbali kwa wanamipango mji wetu. Ukiangalia kwa makini waweza kuona kuwa kituo ni kikubwa lakini katk miaka 5 ijayo kitazidiwa tena. Kumbuka kuna watu wengi wanatumia sehemu hii kupanda mabasi ya mkoani. Sasa ni kwanini hawakutwaa eneo lote lililokati ya barabara ya zamani na mpya?

    Magari yangepangiwa kuingilia katika barabara ya zamani na kuingia kituoni hapo na wakati wa kutoka yatumie mpya. Lakini si hivyo eneo kubwa la hifadhi ya barabara limeachwa na sasa linavamiwa na kituo kitaongeza tu foleni kwani tumeona hivyo katika kituo cha zamani. Tatizo daladala zinapaki mwanzoni mwa kituo kuchukua abiria na zile zinazoingi inabidi zisubiri hadi hawa wajaze na huo ndo mwanzo wa foleni kwani nyingine zinakuwa bado bara bara kuu.

    Observer

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2011

    Observer
    Habari hii ni njema, ila inaelekea katika kituo hiki hakuna public toilet hata ya kulipia? Ajira hiyo wajameni au mpaka tenda itangazwe?
    au tunahitaji muwekezaji?
    Mbezi luis sasa tambarareeeee

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2011

    Sijajua hali halisi ilivyo hapo kituo kipya...lakini mbona naona kama barabara bado ni finyu sana, na kwa hali ya daladala zenye fujo, magari makubwa mengi kutoka mikoani...watu wengi...duh usalama utakuwepo kweli? Mbona sijaona Traffic lights hata moja...au ndo police watageuka kuwa waongoza magari?...Bw. Michuzi hebu muvuzisha picha zaidi za kituo hiki pamoja na barabara nzima ili wadau tuweze kutoa maoni yetu. Mimi sijaridhika bado na hali halisi ya ujenzi huo.
    Mdau Ughaibuni!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2011

    Angalizo langu ni kituo hiki kisipewe Serikali ya Mtaa hapo Mbezi! watakifanya kama kituo kinachotumika sasa kilivyojaa Wamachinga ambao wao Serikali ya MTAA wanachukua hela kila siku na zinaishia MIFUKONI mwao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...