Hi Ankal Michuzi!!
Napenda kutoa shukuran zangu za dhati klwa globu hii ya jamii kwa msaada mlionipatia, Siku ya jumamosi mchana saa saba mwanangu Zuhura Mgweno alinipigia simu na kusema aliambiwa na mwanae kuwa natafutwa na mama yangu kupita blog hii.
Zuhura anasema alipoteza mawasiliano ndio sababu ya ukimya huo,kusema haki nilifurahi kupita kiasi na hapa nilipo nina furaha isiyo kifani jamani,sina la kusema zaidi ya kusema asanteni sana kwako wewe Issa Michuzi na waliotoa maoni wote kwa msaada wenu.
Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea furaha na amani katika maisha yenu.
Akhsante Mdau
Habari kamili za Mama kumtafuta Da'Zuhura
Ankal Michu japo simjui huyu dada, nilposoma habari hii nimefurahi mpaka kidogo machozi yanitoke kwa kuzingatia hisia mama yake alizopitia. Fatma wa Chang'ombe, DSM.
ReplyDeleteSafi sana. Ndiyo maana blog hii ni blogspot ya kwanza katika blogspots zote za TZ kwa kuhudhuriwa (visitors' traffic). Keep it up bro. Mdau wa utafiti wa Information Superhighway Traffic in Africa. (USA).
ReplyDeleteEMOTION..mwili umenisisimka sana jamani kiasi nilie,ankali mungu akupe umri mrefu wenye afya tele ili uweza kuendelea kuisaidia jamii..
ReplyDeleteTunashukuru GLOBU ya JAMII kwa kutumikia JAMII
ReplyDeleteHii BULOGI ya MISUPU inasaidia sana jamani!
ReplyDeleteJAMANI NIMEFURAHI SANA KAMA ZUHURA AMEWEZA KUWASILIANA NA MAMA YAKE..ZUHURA TUNAKUOMBA USIKAE SANA KIMYA UNAWAPA SHIDA WAZAZI..NIMEFURAHI SANA..BLOG YA JAMII OYEEEEEE
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteNilikutumia ujumbe asubuhi kutaka kurekebishwa kwa habari hii. Hii habari ina upotoshaji ndani yake. Katika ujumbe niliokutumia asubuhi nilimuomba huyu Shangazi ajitokeze kurekebisha ujumbe wake.
Zuhura ambaye habari hizi zinapotoshwa juu yake hana uwezo wa kujitetea hapa kwa kuwa ni mlemavu wa kusikia na kuongea.
Huyo anayedai ni Mama yake Zuhura siyo kweli ni Mama yake Zuhura. Zuhura anaishi na Binti yake na Mama yake mzazi mjini Oulu, Finland. Huyu anayejiita Mama yake Zuhura ni shangazi yake Zuhura na wala siyo Mama yake kama anavyodai.
Laiti kama ungemjua Zuhura ambaye huyu Shangazi anamchafua jina sidhani kama ungeacha kuweka maoni niliyokutumia asubuhi.
Nakuomba utende haki kwa kuweka ujumbe niliokutumia asubuhi pamoja na huu ninaokutumia jioni hii.
Asante sana.
Mpaka ukitafuta kwenye mablogg uwasiliane na mama yako aliyekuzaa. Katika dunia ya leo yenye mawasiliano ya kisasa ambayo yako bwerere huniambii kitu you are either insane or out of your mind!!!! Lakini pia nitatoa shukrani kwa blogg.
ReplyDeleteMSEMAKWELI
mungu akubari michuzi japo simwelewi huyo mama na huyo dada lakini nimefurahi sana kusikia amepatikana kupitia blog yako michuzi mungu akubariki sana na kazi yako na nakuombea maisha marefu yenye mafanikio mema najua kupitia glob yako wengi wanafanikiwa n matatizo yao god bless
ReplyDelete