Mtengenezaji Kiongozi wa Filamu ya CHUMO,Jordan Riber (kulia) akiwa na Maafisa wa Benki ya Stanbic ambao ni sehemu ya Wadhamini waliofanikisha utengenezaji wa Filamu hiyo.Kushoto ni Abdulrahman Nkondo na katikati ni Goodluck Chang'a.
Wakazi wa jiji la Dar wakiwa wamefurika kwa wingi katika viwanja vya Biafra,Kinondoni jioni ya leo kushuhudia uzinduzi wa Filamu ya Kiswahili inayoitwa CHUMO ambayo inaelezea athari za ugonjwa wa Malaria wa wanawake wajawazito,iliyotengenezwa na Media For Development International - Tanzania chini ya Uongozi wa Jordan Riber.
Wakazi wa Maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiangalia uzinduzi wa Filamu ya CHUMO katika viwanja vya Biafra,Kinondoni jioni ya leo.
Askari Polisi wakijaribu kuwapanga watu katika utaratibu uliowekwa ili kila mmoja aweze kuona Filamu hiyo.
Pamoja na kwamba kulikuwa na Manyunyu ya mvua ya hapa na pale lakini hakuna alietaka kuondoka eneo hilo la Biafra bila kuitazama Filamu hiyo ambayo ni nzuri na yakusisimua na pia inatoa mafunzo katika jamii kwa swala zima la kupiga vita ugonjwa wa Malaria hasa kwa kila mama wajawazito.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...