Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Mh. John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi nje ya kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar wakiwa wakifatilia hatma ya kukamatwa kwa Mwenyekiti cha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe.
Mh. John Mnyika akiwasilia na simu nje ya Kituo kikuu cha Polisi,jijini Dar mapema leo asubuhi.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Mh. John Mnyika akiongozana na Prof. Abdallah Safari pamoja na mjumbe wa CHADEMA wakiwa nje ya kituo kikuu cha Polisi jijini Dar leo kufuatilia hatma ya Mwenyekiti wao,Mh. Freeman Mbowe anaeshikiliwa na Jeshi la Polisi hivi sasa.
Mawasiliano ya hapa na pale yakichukua nafasi kwa viongozi wa CHADEMA leo asubuhi.
Ulinzi mkali katika kituo kikuu cha Polisi Dar es salaam leo,alikoshikiliwa kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe.
Wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wakiwa nje ya Kikuo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam mapema leo asubuhi ambapo walifika ili kujua hatma ya Mwenyekiti wao ambae pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe.Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2011

    mungu wangu! akina ras makunja nao wapo na magitaa yao,tayari tayari kuanza mziki??????

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2011

    Mie kama wamemkamata bila ya makosa basi ni dhambi kubwa ila kama kafanya kosa basi kukamatwa ndio inavyotakiwa kwasababu yeye ni mmoja ambae anaezitunga hizo sheria ikisha avunje sheria ya kutoenda mahakamani au hata kumpeleka mdhamini wake ni vibaya kwasababu yeye ndio kiongozi anatakiwa awe mfano mzuri kwa wananchi hiyo kwa kiswahili sahihi ni dharau. Hukumu ndio haki yake na lakini isiwe kwa Chadema tu hii adhabu iwe kwa mtu yoyote bila ya kuangaliwa usoni ndio hapo maendeleo yatakapopatikana i wish nije kuwa kiongozi wa hii nchi manaake kuna watu wanajifanya hii nchi kama yao kwahivyo hata wakifanya kosa wanakuwa untouchable. I WISH
    Mdau

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2011

    Polisi acheni kuwanyanyasa wapinzani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2011

    Justice shall be done

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2011

    Sheria ifanye kazi yake na tumwogope Mungu kutekeleza hili kwa manufaa ya nchi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...