Waziri wa Kilimona na Mali Asili,Zanzibar.Mh. Mansoor Yussuf Himid
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

WAZIRI WA KILIMO MALI ASILI MHE MANSOUR YUSSUF HIMID AMESEMA MIPANGO YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA HADI IFIKAPO MWAKA 2015 HEKA 6000 ZIWE ZINALIMWA NA KUZALISHA MPUNGA ILI KUPUNGUZA UAGIZAJI MCHELE KUTOKA NJE.

MHE MANSOUR AMEELEZA HAYO HUKO WIZARANI KWAKE DARAJANI ALIPOKUWA NA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDONESIA NCHINI TANZANIA YUDHISTIRANO SUNGADI

AMESEMA SERIKALI ITAHAKIKISHA INAWAWEZESHA WAKULIMA ILI KUFANIKISHA LENGO HILO HALI ITAKAYOWEZESHA WANANCHI KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA.

AMESEMA HALI YA UZALISHAJI MPUNGA ZANZIBAR HIVI SASA HAIWIANI NA MATUMIZI YA MCHELE AMBAPO WAKULIMA HUZALISHA TANI 16 KWA MWAKA KIASI AMBACHO HAKIKIDHI HATA ROBO YA MAHITAJI YA WANANCHI WA ZANZIBAR.

NAE BALOZI WA INDONESIA NCHINI TANZANIA BWANA SUNGADI AMESEMA SERIKALI YAKE IMELETA WATAALAMU WAWILI ILI KUSAIDIA TAALUMA KWA WAKULIMA NA KUWEZA KUZALISHA MPUNGA KWA WINGI NA WENYE VIWANGO .

AMESEMA WATAALAMU HAO WATAWEZA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MBOLEA ISIYO NA KEMIKALI ILI KULINDA AFYA YA MLAJI PAMOJA NA UHARIBIFU WA ARDHI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2011

    wizara ya Kilimo ina tatizo kubwa ya uendelevu wa Miradi, Kwa miongo kadhaa wametepata miradi mikubwa sana kutoka FAO na mashirika mengine. Wafadhili wakiondoka tu, kila kitu kinalala. Wizara ilikuwa na kitengo imara sana cha elimu kwa wakulima na vitendea kazi (studio na watendaji). Jee leo hii wako wapi? Khamis na team yake wanafanya nini.
    Ushauri: Wizara ijipange kimkakati, waweke mpango endelevu wa kilimo, wawawezeshe wasomi wake kwa nyenzo na motisha. Mshahara wa Masters graduate leo hii ktk wizara ya Kilimo unalingana sana na Mwalimu mwenye degree ama wafanyakazi wa afya wenye Diploma ama Vijana wa Vikosi vya SMZ. Heshima iko wapi ya msomi?.
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...