Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatarajia kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuboresha huduma kwa Wanachama na hasa suala zima la uboreshaji wa upatikanaji wa Vitambulisho vya Wanachama kwa Wakati.

Hayo yalisemwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bwn Hamis I.Z. Mdee wakati akifungua mafunzo ya siku tatu (3) ya uboreshaji wa huduma kwa mteja kwa Watumishi wa Idara ya wanachama inayofanyika katika ukumbi wa Amabilis mjini Morogoro.

Amewataka watumishi wa Mafunzo hayo kuwa wabunifu na wenye kujituma katika kuwahudumia wanachama na wadau mbalimbali na hasa katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha, amewataka watumishi hao kuzielewa changamoto mbali mbali zinazoukabili Mfuko huo likiwemo suala la kukua kwa kiteknolojia sambamba na majukumu ambayo Serikali imeyakasimu kwa NHIF yenye lengo la kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

“Suala zima la undaaji na usambazaji wa Vitambulisho vya matibabu kwa Wanachama bado ni changamoto kwa hiyo lazima jitihada za makusudi zifanyike ili kuondoa Changamoto hizi” Alisema bwana Mdee.

Amesema, kwa mwaka ujao wa fedha Mfuko umeandaa mikakati maalumu kwa kuwekeza katika kuimarisha mifumo ya habari (ICT) ili kuongeza tija na ufanisi wa majukumu ya Mfuko ikiwemo suala la undaaji na usambazaji wa Vitambulisho vya wanachama.

Bwana Mdee, amesema Mfuko umejiwekea lengo la kufikia 30% ya Watanzania wote ifikapo mwaka 2015. Kwa sasa Mfuko huu unahudumia wanachama 15.4% ya watanzania wote. “ Ni lazima Wananchi wakaelimishwe na kushawishika kujiunga na Mifuko hii ya CHF na NHIF ili lengo hili liweze kutimia” amesema Bwana Mdee,

Mafunzo haya yana lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa Idara ya uanachama kwani ni kiungo muhimu katika kuwapa huduma wanachama wa Mfuko na wadau mbalimbali na umewahusisha viongozi waandamizi kutoka Ofisi za Kanda za Mfuko huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...