Mjomba Ankal,Salamaleko

Nimatumaini yangu uko poa, pole na kazi , maana shughuli hii si mchezo.

Mimi kama mdau wa globu hii, napenda nitumie nafasi hii kuwajuza watanzania hususani wanafunzi wanaotaka kujiunga na baadhi ya vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.

Chuo Cha Uhasibu Tanzania, kaka ulishapata nafasi hata siku moja ukakitembelea ? binafsi huwa sipendi hata marafiki zangu waje kunitembelea chuoni hapa maana naona aibu.

Chuo wanachotoka wahasibu wa Tanzania kaka kina mazingira machafu sijapata ona ,ni kama shamba la kufugia kuku, mbaya zaidi mtaro unaotoka katika Canteen ,unaotoa maji machafu umefungwa hivyo maji hayo yametuama hayaendi kokote, hivi sasa kuna inzi wengi ajabu, mbu ndio usiseme,Wakati wenzetu wa Wizara ya Afya wanasema MALARIA HAIKUBALIKI, Ankal chuo cha TIA kinasema MALARIA NA KIPINDUPINDU VINAKUBALIKA, Eneo linalokaliwa na wanafunzi zaidi ya elfu moja, wameshindwa hata kufanya furmigation, chuo kinachomilikiwa na Wizara ya Fedha, mazingira kuwa machafu.

Inaathiri hata uelewa wetu sisi wanafunzi, wadau wa globu hii labda muwakumbushe viongozi wote wanaohusika na masuala ya mazingira kuanzia ngazi ya kata mpaka huko juu, labda tutaona tofauti maake tumeshasema na uongozi wetu tumechoka, nitakutumia picha ya maeneo hayo ujionee mwenyewe.

Mdau 
Mwanafunzi wa TIA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2011

    Mdau duh sielewi? hivi kusafisha mazingira yako unayoishi mwenywe ni mpaka serekali ijekuwasafishia?. Kwanini hamwezi kufanya wanavyosema wenzetu harambee nyinyi wanafunzi kusafisha mazingira yenu, na ndiyo muitafute serikali ilete hiyo gari la kebeba taka? kama mtasubiri mpaka serekali itume watu kuja kuwafagilia itakuwa siyo maendeleo tena wakati wachafuaji wa mazingira ni nyinyi wanafunzi wenyewe... noma. Jikusanyeni wanafunzi na fanyeni mazingira yenu yawe ya afya kwenu na watakaokuja kuwatembelea. It all starts at home. Kujitolea na kuweka mazingira yenu safi hayategemei tu serekali jamani duh...changamkeni bwana wenzetu ugaibuni mazingira ya kwenye jengo kubwa la kuishi flat yanasafishwa na wanaoishi kwenye flati hizo, na serekali inaprovide kubeba kwa taka...duh noma kusubiri msafishiwe uchafu manaoufanya wenyewe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2011

    Kwani wewe upo hapo kwa kufuata mazingira au kusomea uhasibu. Enzi zetu tukienda vyuoni ilibidi kwanza tupitie JKT mwaka mzima. Tunalima na kulinda nchi, wakati huo niliponea chupuchupu kwenda katika vita vya Kagera. Sasa vijana wa siku hizi mnapewa elimu bure na mikopo juu, bado kitanda utandikiwe. Acha wewe, ndio maana mafisadi wengi hii nchi. Mazingira yanawekwa kwa usafi na watumiaji wenyewe sio usubiri wizara iajiri wasafishaji. Mkuu wa chuo anatakiwa akupangieni Jumamosi na Jumapili ni siku za kuweka mazingira katika hali ya usafi sio kwenda disco au twanga pepeta. Kama hamuwezi kuweka usafi mazingira yenu nyinyi wenyewe wakaazi basi lipeni kwa wasafishaji, sio msubiri walipa kodi wakulipieni. Ndio maana miprofesa mingi ni mifisadi. Wenzenu wa ughaibuni wanasoma huku wanabeba maboksi usiku mzima.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2011

    weka picha mambo yawe mwake ...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2011

    Ingawa sijaelewa ni chuo kipi, nadhani ni kile cha kurasini hapo Bongo.
    Bwana Michuzi, mwenyekiti wetu wa blog hii ya jamii naomba sana ufuatilie jambo hili ili upige picha za maeneo machafu na kuzirusha haraka.Nchi yetu ipo pabaya sana hasa hali ya maisha ya wananchi ikiwa ni pamoja na wanafunzi wetu. Fedha inayoidhinishwa inaenda wapi? Kama kiongozi anabadilika gafla kimaisha na kuwa juu wakati alikuwa chini kabla ya cheo na kamshahara kale kale. Matumizi sh.1,000,000/= kila mwezi hali kamshahara kake ni sh.300,000/=. Je, hizi anazipata wapi kiongozi huyu? Ushauri wangu ni huuuuuuuuuuuu...... anzani mgomo haraka
    enyi vijana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2011

    Bongo kama New York.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2011

    mdau hapo juu nadhan hujaelewa, ishu sio kufagia na kuweka mazingira safi, tatizo ni maji machafu yanatiririshwa ovyo!kuna kibwawa cha maji hayo kati ya bwen la wadada na lecture hall yaani ni aibu. subiri picha ziwekwe mjionee maajabu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...