Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua Semina ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kwenye ukumbi wa St. Gaspar Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Capt. George Mkuchika baada ya kufungua semina ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kwenye ukumbi wa St. Gasjini Dodoma Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo PInda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paschal Mabiti baada ya kufungua semina ya Wakuu wa Mikoa ,Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kwenye ukumbi wa St. Gaspar Mjini Dodoma leo.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri Mkuu, MIzengo Pinda wakati alipofungua semina yao kwenye kukumbi wa St. Gaspar Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakitoka kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma baada ya Waziri Mkuu kufungua Semina ya Wabunge kuhusu Taasisi ya Uongozi Institute . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


nimependa sana picha ya hapo mwisho, mtoto wa mkulima kapedeza sana na mama makinda, duhh yaani duniani watu wanaumbwa.
ReplyDeleteUkisikia serikali zinazonyonya wananchi ndo hizi. Sasa Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa mkoa, kuna Mkurugenzi mtendaji wa Mkoa, Kuna Mkuu wa wilaya, Katibu tawala wa wilaya, Mkurugenzi mtendaji wa wilaya..halafu kuna wengine wengi sijui afisa mipango, Afisa Elimu, Misitu...na kuendelea..hivi hawa watu wote huko wilayani wana kazi kweli? Mbona mnatumia mapato ya serikali kwa njia hii? Kuna ngazi nyingine nyingi tu sijui kata, tarafa, kijiji na wabunge na madiwani na bado hawa wote hawawezi kutuletea maendelea badala yake wanakuwa tu mzigo kwa taifa. Hebu fanyeni namna mrekebishe hiyo organization chart...punguzeni hao watu kwa kuwapa majukumu zaidi na malipo zaidi wachache. Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wanatosha kabisa kwenye ngazi ya juu ya wilaya.
ReplyDeleteAnony wa pili umenifurahisha sana. Nafikiri sasa wananchi mnaanza kuona ubovu wa uongozi wetu. Hili jambo uliloongea CHADEMA walishaliongea wakasema watapunguza hizo safu ili wale wasio na tija waondoke wakafanye kazi zingine. Siwapandishi chati Chadema lakini pale mtu anapokuwa na mawazo ya kimaendeelo tusimkatishe tamaa eti kwa sababu "AHH jama fulani ana sifa zooote lakini mmmh jama Mkara! Sifa zoooote anazo lakini Mkara?" Sasa sisi wengine tuliopiga kura nasikia tulikuwa tunasema fulani ana sifa zooote lakini mmmh jama Mkiristo? Au Mmm jama Muislamu?" Wengine wakaangalia anatoka kanda gani. Haya ndugu zangu watanzania hayatatujenga.
ReplyDeletesafi sana wadau wote mmeongea point tupu.....big up watanzania kwa kuanza kuamka kielimu na kiupeo.
ReplyDeleteMimi ndiye mdau wa pili nashukuru kwa wote mlioona kuwa I make sense. Sasa ngoja niwape zaidi...kuna watu kama Mkandarasi wa wilaya (Ati District Engineer), hivi kuna miradi mingapi wilayani inayohitaji full time district Engineer? na chini yake ana ma technician sijui wangapi. Tangu lini mkahitaji district engineer kujenga madaraja yanayotumia mapipa? Halafu hata huko walipo lami hakuna sasa kazi yake ni nini? Kusimamia ma-grader yanayosawazisha udongo? Haya kuna mtu anaitwa sijui District water officer na bomba za maji anazosimamia unaweza kuzihesabu na most of them hazina hata maji. Na hao sijui Mwenyekiti wa Council wana kazi gani? sijui ndo wasimamizi wa madiwani? Na wabunge wanasinzia tu na kudai posho. Hivi mnatufanya sisi wajinga kiasi gani? Watu wooote hawa na hakuna maendeleo, mimi nadhani ni kwavile hakuna anayejua majukumu yake na wote wanategeana tu. Ati nilisikia story mkandarasi wa wiliya anasimamai ujenzi wa Clinic. Jamani ujenzi wa Clinic hiyo hata Mwenyekiti wa Kijiji anaweza kusimamia. Kwani hiyo clinic inakuja na OR (operation room)? au ni ya gorofa? si ni vyumba tu kadhaa? Jamani tumechokaaaa...!! Mdau, CA-USA
ReplyDelete