KUNANI TRA IDARA YA KULIPIA MAGARI YANAYOINGIA???
Mimi ni Mtanzania ambaye nafanya kazi kwenye taasisi moja hapa nchini. Baada ya kujibana sana niliweza kuagiza gari na limefika. Kwa muda wa siku kadhaa sasa najitihada za wakala wangu hadi sasa sijui kinachoendelea, lakini nyepesinyepesi ni kuwa TRA wamebadilisha system yaulipiaji magari ambayo ndiyo imesababisha huu usumbufu.
Mimi kamaMtanzania, najiuliza je TRA, inayohitaji kukusanya mapato mengi ilikutukomboa kwenye umaskini inakatisha tamaa walipaji kodi kwa ucheleweshaji wa makusudi!.
Natumaini blogu yajamii ni njia bora ya kuliweka
hili wazi na tukipata ufafanuzi wa TRA utaleta ahueni.
Mdau Kigamboni


aise we acha tu nna wiki 2 naambiwa system znafungwa huku bandari wanaesabu storage na garama ziko juu ukilinganisha dolla ilivo sasaivi inasikitisha sana maisha ya mtanzania yanazidi kuwa magumu kila siku ushuru pia umepanda maradufu
ReplyDeleteyaan kaka pole tra hizo ndio zao hamna watu wa rushwa kama hao bila pesa gari halitoki watakwambia makaratasi hayaja pita bado oh namany more lakin ukiwapa pesa tu gari utatoa dakika so just wape pesa ya moto .watu wote wanao toa magari wawe wanawapa pesa ya moto hapo ndio wataacha kuchukua rushwa.
ReplyDeleteWewe unayesapoti rushwa una mawazo finyu kweli kweli. au unafanya kazi TRA? Haki haipatikani kirahisi. Mkiwapa rushwa ndio mnawafanya waone huo ni utamaduni wao hivyo asiye na pesa hatapitishiwa gari lake. Vumilia tu kaka.
ReplyDeleteMimi lakini nilitoa gari pale mara mbili kupitia kwa agent wangu haikunichukua muda mrefu. gari ya kwanza ilinichukua kama siku nne tangu iingie bandarini ambapo ya pili ilinichukua kama wiki moja.
ReplyDeleteMichuzi tunashukuru ulivyobadilisha utaratibu wa kuingiza maoni na kutuma. Sasa hivi ni rahisi sana na meseji inakwenda kiurahisi. Yaani umetuchanulia sisi kazi yetu ni kuingiza tu na kutuma.
ReplyDeletekwa kweli TRA wamezidi sana ni mateso makubwa kutoa gari utasubiri release mpaka uchoke ila ukitoa tu pesa basi mambo shwari
ReplyDeletetra wamekuwa miungu watu mbona mamlaka nyingine husika kama ticts , bandari,icd's na cfs hawana usumbufu kama wao? wabadilike mimi naamini ukiwepo usimamiz mzuri ipo kodi ya kutosha ukizingatia nchi zaid ya tano wanapitisha karibu kila kitu pale dar na uchumi wao wakua why not us tuwe strategic kwamba hii gate way ya nchi zote hizo itumiwe vizuri kukuza uchumi wahusika mnajua lakini sijui inakuwaje!
ReplyDeletebora watu waendelee kutoa rushwa tuu ndio short cut
ReplyDeleteTRA Fanyeni kazi yenu kwa mujibu wa sheria mambo mengine achaneni nayo
ReplyDeleteDavid V
Hii ya kutoa maoni kwa mtindo huu iko sawa kaka Michuzi hapo timeelewana!
ReplyDeleteNdio maana Mheshimiwa Mkapa alitimua kazi wote. Nyie hamuoni maisha wanayoishi mitaani. Ni rushwa kuanzia hizo ndogo na mpaka kubwa. Tusiseme mengi ila hao ndio wenye hii nchi. Wananitia hasira sana. Hivi ni nchi zote ukifanya kazi TRA basi wewe unakuwa na gunia la fedha chumbani. Maana nasikia wanaogopa benki watakamatwa na PCCB. No wonder tutakuwa masikini milele
ReplyDeleteTesting uharaka wa maoni kupostiwa hapa
ReplyDeleteHahahahaaaa mdau umenifurahisha kweli. Kwa taarifa yako wewe na wadau wapendwa wengine ni kwamba Globu ya Jamii hailali, timu ina shifti nne za 24/7 nadhani umejionea mwenyewe na hiyo 'testing yako'
ReplyDeleteHahahahhh
ReplyDeleteNi nadra sana Ankal kuandika maoni, ahsante sana. Tunashukuru kama unazingatia maoni yetu, sisi ndo wamiliki haswa wa globu. We are why you blog! Big up sana Ankal