Ankali naomba ufikishe kilio chetu sisi wanafunzi watumishi,
Sisi ni wanafunzi ambao ni watumishi katika idara, taasisi na halmashauri mbalimbali ambao tunasoma Post graduate Diploma in procurement and Logistics management hapa katika Taasisi ya Uhasibu Tanzanian (Tanzania Institute of Accountancy - TIA).
Naamini ilikuwa lengo zuri tu la serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kuongeza ujuzi kwetu sisi wataalamu wa sekta ya manunuzi ambayo inachukua 70 percent ya bajeti kuu ya serikali, ili kuachieve value for money concerpt, lakini mambo yanaenda kinyume kabisa badala ya kutuongezea ujuzi sasa imebadilika na imekuwa kutuongezea shida na karaha kwa mateso tunayoyapata kutokana na kutolipwa stahili zetu kwa wakati.
Tunaomba ufikishe kilio chetu kwa Mdhamini wetu(sponsor) yaani Mhasibu Mkuu wa Serikali (ACCOUNTANT GENERAL) kwa kuchelewa kutulipia fedha zetu za field pamoja na chakula kwa wakati muafaka. Hii leo tunaongea tunasikia malipo ya serikali yatasitishwa wakati wowote wakati hapa tulipo tayari tuna Proposal ambazo tunatakiwa tuende field tukafanye reasearch lakini mpaka sasa hivi hakuna dalili za malipo hayo. Kuna Kamati ya wenzetu tuliichagua wakafatilie lakini kila wakienda wanagonga mwamba wahusika mara hawapo na vitu kama hivyo.
Hapa tulipo tuna karibia kufanya mtihani wa mwisho wa kumaliza semister ya pili lakini hakuna dalili yoyote ya malipo hadi tunajiuliza tumefanya kosa gani mpaka tuteseke hivi ? Tumepunjwa malipo ya posho ya chakula pamoja na chuo kutoa ushirikiano ili tulipwe lakini hadi leo kimya, hivi ni kweli tunayofanyiwa haya sisi watumishi ? Kwanini tusinge dhaminiwa na waajiri wetu kama Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali iliona kwamba haitaweza kutugharamia na kwanini tuliandikiwa barua kwamba gharama zote zitalipwa na mdhamini ambae ndio yeye Mhasibu mkuu wa serikali ? Hivi na sisi na utuuzima wetu huu tubebe mabango kwa maandamano na migomo ? Sisi tunaamini mtumishi wa Umma ni kioo. Sisi maandamano hatuyawezi lakini mamlaka husika ilione ili. Hata kama lawama nyingine ni za Management ya Chuo lakini sisi hatustahili adhabu hii jamani.
Chonde Mhasibu Mkuu wa Serikali tunakuomba utuokoe TUNADHALILIKA. Tujitahidi jamani kuipunguzia serikali mzigo wa kujibu hoja na malalamiko yasiyo na sababu ambayo yanatokana na watu fulani kutotimiza wajibu wao katika nafasi zao walizopewa.
Sisi tunaamini kilio chetu kitasikilizwa kwa wakati ili tuapate posho zetu za chakula na Field.
Mungu Ibariki Tanzania
Ni sisi wanalibeneke wenzako wa TIA
Mara nyingi huwa nakuwa sipendelei wanafunzi wanaodai fedha za field au reserch kulazimisha kila jambo kama ni haki yao kwanza kupata fedha kutoka seriklini na wengine kama walio ma-hospitalini,wanaotibiwa kwa fedha za serikali kuacha wafe ili mwanafunzi wa UDSM au UDOM au TIA aende field.
ReplyDeleteLakini leo , nitakubaliana na huyu wa TIA, kwamba kugoma na uzee huu hakuna heshima ila hili swala lao lipewe kipaumbele kiu-ungwana.
Mdau tunataka watu kama nyinyi mnao-elewa nini mmekuja kusomea na miundo ya fedha za serikali zinatoka na kufanya kazi vipi, kwani nyinyi ndio wasimammizi wa fedha hizo mkimaliza kusoma hizo Post-graduate zenu.
Serikali iwasikilize shida zenu na kuwapa haki zenu. Vyuo vyote vingekuwa hivi tungekuwa na wasomi wa maana na baadaye wafanyakazi wa maaana.