WAZIRI wa habari Utamaduni 
Utalii na Michezo Abdilah Jihad Hassan
Na Mwandishi wa Idara ya Habari,Zanzibar.

WAZIRI wa habari utamaduni utalii na michezo Abdilah Jihad Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Iran kubadilishana wataalamu katika fani mbali mbali na kuwapatia mafunzo ya uandishi wa bahari waandishi wa habari wa Zanzibar.

Amasema kuna haja kubwa kwa Serikali ya Iran kubadilishana wataalamu na kuwapatia waandishi wa habari wa Zanzibar mafunzo ili waweze kuijengea uwezo taaluma yao wanayoifanyia kazi.

Waziri Jihad alisema hayo leo huko ofisini kwake Kikwajuni wakati alipokuwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa sinema na masuala ya televion wa Iran Javad Shamaqdari pamoja na ujumbe wake.

Akizungumzia juu ya suala la utamaduni wa Zanzibar Waziri jihad alisema kuwa Utamaduni wa Zanzibar na Iran ni Tamaduni ambazo zimeingiliwa na Tamaduni nyengine jambo ambalo limepelekea kuharibika kwa utamaduni huo

Hata hivyo Waziri huyo wa habari wa Zanzibar alisema kuwa mipango inafanywa ili kulipatia ufumbuzi suala hilo la kuchafuliwa kwa tamaduni zetu ambazo zinalingana kati ya Jamhuri ya Iran na Zanzibar.

Aidha alisema mbali ya kulipatia ufumbuzi suala hilo pia kuna haja kubwa kwa Serikali ya Iran kushirikiana na Zanzibar katika Nyanja ya masuala ya utalii.

Naye Naibu Waziri wa Sinema na masuala ya Televion wa Jamhuri ya Iran Javad Shamaqdari amesisitiza kuwepo na mashirikiano kati ya Zanzibar na Iran katika masuala ya Utamaduni na Habari.

Alisema ipo haja kubwa kwa nchi hizi mbili kuimarisha na kudumisha mashirikiano katika Nyanja hizo ambazo zinahusiana na masuala ya Habari na Utamaduni.

Akizungumzia juu ya maoyesho, Naibu Waziri huyo alisema kuwa Jamhuri ya watu wa Iran wanayo maonyesho yao ambapo hata hapa Zanzibar yapo lakini alisema kuna haja ya kuanzishwa maonyesho ya Shirazi Festival.

Akizungumzia suala la makumbushoNaibu Waziri huyo wa Iran alisema wanayo makumbusho yao lakini katika hili alishauri kuwa kwa hapa Zanzibar kuwepo na makumbusho ambayo yanaelezea kwa uwazi kwa kitu maalumu ambacho hakikupi taabu unapofika hapa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2011

    Jamani tunapoongelea tamaduni si vitu ambavyo tuliletewa na wakolonoi yaani wazungu na waarabu, tamaduni ni yale mambo ya asili tuliyokuwa nayo kabla ya wakoloni, enzi hizo hakukuwa na mambo ya mwanamke kujifunika mwili mzima utadhani anataka kujilipua mhanga, wazungu ndio waliokopi tamaduni zetu na sasa wanaziita zao, sisi ndio tuliokuwa hatuvai nguo yaani mambo yalikuwa kama kwa mswati sasa hivi ukifanya hivyo unaonekana unaiga western.
    iweje mheshimiwa aseme utamaduni wa zenji unafanana na wa iran hayo ni mapokeo tu. ukiongelea utamaduni kweli hakuna mfanano hata kidogo.

    michuzi hata ukibana message sent
    kwa heri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...