Waziri wa Katiba na Sheria
Mh. Abubakar Khamis Bakar
Na Idara ya Habari Maelezo - Zanzibar.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Bajeti hiyo imepitishwa na Wajumbe leo mchana bila mabadiliko. Awali akitoa majumuisho ya michango mbalimbali ya Wajumbe waliochangia, Waziri wa Wizara hiyo, Abubakar Khamis Bakar ameliambia Baraza kwamba kwa sasa hakuna mchakato wa kuandika katiba mpya.

Waziri Abubakar amesema kazi iliyopo kwa muda huu ni kuweka kanuni na uwanja sawa kwa wananchi kuweza kutoa maoni yao namna wanavyotaka wakati ukifika wa kuandikwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati Baraza lilipokaa kama Kamati ya Matumizi ikihusisha Baraza zima, hoja mbalimbali kutaka ufafanuzi zilijitokeza zaidi ikigusa mchakato wa kuandika kwa Katiba mpya ya Tanzania.

Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe(CUF),Ismail Jussa amehoji nafasi ya Baraza la Wawakilishi katika mchakato wa kutungwa upya kwa Katiba ya Tanzania ambapo Serikali imesema kila kitu kina utaratibu wake na kwa sasa maandalizi yote yapo chini ya Wizara ya Katiba na sheria.

Amesema kwa mujibu wa mkataba wa Muungano wa mwaka 1964, kazi ya kuandikwa kwa Katiba mpya ni ya Bunge la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,lakini wananchi kabla ya kufikishwa mbele ya Bunge hilo watapewa nafasi ya kutoa maoni yao.

Waziri huyo amesema wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Wizara kama hiyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo hauwezi kulitaka Baraza la Wawakilishi kusimamia jambo hilo kwa sasa.

Amesisitiza kwamba jambo hilo litakapokuwa tayari litawasilishwa katika Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kupata maoni ya Wajumbe wa Baraza hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...