Mwenyekiti wa kampuni ya kufua umeme ya Syimbion Power ,Africa Bw Joe Wilson akizungumza jambo na waandishi habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA |
Picha na Habari na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii
Akizungumzia ugeni huo balozi Maajar amesema wakuu hao wa kampuni mbalimbali zaidi ya 17 wamekuja nchini kuangalia maeneo ambayo wataweza kuwekeza hususani katika sekta ya nishati,Kilimo,Usafirishaji na utalii.Amesema ujio huo umeandaliwa na ofisi yake ukijulikana kama V.I.P SAFARI ambapo leo mchana watakula chakula cha pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wa mjini Arusha yaani Business Lunch na baadaye watakutana na mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Isdor Shirima kwa ajili ya chakula cha jioni.Amesema wakiwa nchini wageni hao watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii kabla ya kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya maonesho ya Saba saba na baadaye kula chakula cha pamoja na rais Jakaya Kikwete.Balozi Maajar amesema pia wageni hao watatembelea Zanzibar ambapo watakuwa wageni wa rais wa Zanzibar Dk Ally Mohamed Shein ambapo pia watapata fulsa ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya
utalii katika mji wa Zanzibar.
Naona mama katuwakilisha watanzania kwa vazi zuri. Hiyo ndiyo maana ya balozi au siyo Michuzi?
ReplyDeleteMdau mafichoni