Jana niliona comments mbalimbali zinazoonyesha watu hawana habari hata na kitu kinaitwa mabasi yaendayo kasi kama ilivyo hapa Jakart, Indonesia. Hiyo picha inajieleza. Kama mtu bado tu hataki kuelewa na ubishi wake wa Kibongo, ni kwamba njia za mabasi yaendayo kasi kwa ajili ya mabasi hayo tu. Ni kosa la jinai kupitisha gari ama pikipiki katika njia hiyo. Mpo hapo waosha vinywa??
-Mdau Jakarta

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2011

    Hiyo ni barabara inayotumiwa na mabasi. Mdau kiswahili tu watu kinawapiga chenga. Umeeleweka na umefanya kazi nzuri ya kutuonyesha picha. Tatizo ni kiswahili kasi ni mwendo mkubwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2011

    Katika nchi zingine hizi barabara zinaitwa HOV yaani unatakiwa uwe na abiria kwenye gari ndio unaruhusiwa,maana inapunguza kila mtu kuendesha gari yake peke yake,na hii barabara(same lane-single or double) huwa inatumika kwenda na kurudi mjini ,asubuhi na jioni respectively(<>)

    http://en.wikipedia.org/wiki/High-occupancy_vehicle_lane

    ReplyDelete
  3. yeah thats the bus lane...au tunaweza sema barabara ya basi pekeeyake..mbona ughaibuni zipo nyingi sana...sasa kwetu kuna lane moja ,tutaweza wapi kuwa na bus lanes jamani...tujikune tunapoweza jamani

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2011

    unamaanisha nini ukisema kuwa mabasi yaendayo kasi? sio kasi wewe mdau ni kuwa tu haina foleni!!! hakuna kusimama hivi unafikiri mabasi yataendaje kasi kwa hiyo barabara? kwanza fikiria wewe mwenyewe hapo ni town na hakuna gari inaenda kasi mjini kuna speed limit... elewa unachokifanya huko acha kuparamia vitu its public transport lazima iwe na njia ya pekee elewa kwanza na ujuwe hiyo njia pia ni ya emergency kama police, ambulance na fire fighter.. tatizo la watanzania ni umasiki wa akili pia tunao.. utaona watu wanashabikia na ndio maana hatuendeleiiiii....... ukijuwa nini maana yake na wewe utafanya kama hujuwi utabaki kushabikia tu.. umasikini na ushamba ni kitu kibaya sana

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2011

    In early 1960s, the level of economy between East Africa and countries such as Malaysia, Indonesia, and Singerpore was almost the same. Bad enough, the timing for independence was almost the same. Now, how comes wenzetu wana kimbiawakati sisi bado tunatambaa? What went wrong? Is it our education that makes us rely on Kuwezeshwa? Kwani inahitaji sayansi ya roketi kugundua watu watatu wanaoendesha magari tofauti kutokea kimara kwenda posta, mmoja anataka kunua stamp, mwingine ku-post barua,na watatu kuchukua barua.If we had a post office at Kimara we would eliminate those unnecessary three vehicles. Do we need foreign kuwezeshwa fifty years after independece for a simple logic like that. What'up with our critical thinking and reasoning? Is our education relevant any more? Now we are talking about high speed buses, but under what perception do we define "high speed"? For God's sake, if at all ,we come up with such definition,which roads in Dar will accomodate such speed? God bless Tanzanian EDUCATION. (Sorry for swanglish)

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2011

    zileteni bongo halafu muone madereva wa daladala watakapozifanyia kazi,labda muwafunge wote mtakao wakamata wanapita huko bila hivyo na foleni za bongo jipangeni kabisa kuzikuta daladala huko na foleni juu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2011

    safi sana unafikiri kwa mpango huo kuna mtu atataka kutumia usafiri wake kufika mjini na wakati anajuwa basi litamfikisha haraka kazini na haraka kurudi nyumbani wakati ukiwa na usafiri wako utakesha kwenye foleni

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2011

    Mdau hapo juu, tofauti kubwa ni mtazamo....huu upuuzi unaitwa Heshima Business hadi kwenye vitu ambavyo mtu anatakiwa awe professional. Tunamhitaji mtu kama Lowassa, basi!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2011

    Fikirieni. Gharama za hiyo DART ni mara 3 ya deni la nje la Taifa. Halafu tunaambiwa inabidi waandae na mipango mingine maana hiyo ya dart ni ya miaka 5 tu. Ni ufisadi au? Wenzetu wanaprogram za miaka 50!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2011

    NYINYI WADAU WOTE MLIO COMMENT HIVI MNAPENDA KUJIFURAHISHA AU MKO MNAOTA? HIYO HABARI YA BUS LANE BONGO HAIWEZEKANI KWA HIYO ACHENI NDOTO MBAYA MBAYA. Mdau toka BUJA

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2011

    Mdau wa JAKARTA wasikuumize kichwa hivyo vitu vya kawaida katika nchi zilizopiga hatua mbona hata SAUZI zipo bwelele

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2011

    MDAU UKO JARKATA TU LAKINI UTADHANI UKO NEW YORK? WENZAKO WA MAJUU WAMEANZA KUZIONA HIZO MIAKA KIBAO ILIYOPITA LAKINI WEWE KILA SIKU BARABARA HIZO ZIKO MDOMONO MWAKO ZILIKUSHANGAZA SANA NINI MARA YA KWANZA ULIPOZIONA? VIPI NA YALE MADARAJA YA JUU (FLY OVER) MDAU HUJAYAONA NINI HUKO? KAMA UMEYAONA TUELEZEE BASI NA HAYO MAANA YAKO MENGI HUKO.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 04, 2011

    Hizo nchi zenye bus lanes ziko well regulated Kampuni za basi ni moja au mbili na mabasi yanasafiri kwa muda. Hebu fikiria ukiwa kwenye single lane halafu mbele kuna basi linasubiri lijae abiria ndio liondoke. Hiyo foleni itakuwa better than now au worse?

    Ili hilo liwezekane unahitaji kuleta UDA back na uban private buses.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...