Meneja wa Mafunzo na Maendeleo wa Benki ya Exim Tanzani, Priti Punatar (kushoto) akitoa mada katika mafunzo ya ndani ya siku moja kwa wafanyakazi wa benki hiyo  yanayobeba ujumbe wa ‘Ugunduzi ni Maisha’ chini ya programu ya ‘eMpower’ kwa lengo la kuwaongezea uwezo na ufanisi katika utendaji wa majukumu yao ya kibenki. 

Na Mwandinshi Wetu


Benki ya Exim Tanzania imezindua programu maalumu ya mafunzo kwa wafanyakazi wake yanayojulikana kama ‘eMpower Program’ yakibeba ujumbe wa ‘Ugunduzi ni Maisha’ kwa lengo la kuwaongezea  na kuwajengea uwezo katika kumudu majukumu yao ya kila siku.


Mwenyekiti wa Benki hiyo, Yogesh Manek alisema Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kuwa Benki ya Exim inaamini kuwa ubora na mafanikio wa malengo yao ya kifedha yanategemea uwezo wa wafanyakazi wake.


 “Ujenzi wa uwezo wa ufanyajikazi ndani ya benki yetu ndiyo nguzo pekee itakayoleta ufanyajikazi wa pamoja na unahitaji mfumo mzuri wa uongozi ambapo mafunzo na maendeleo haya ni sehemu ya mipango ya nguvu kazi  na hii ikatusukuma kuanzisha kituo cha mafunzo ya wafanyakazi wetu mwaka 2008”, “Kituo cha mafunzo cha benki kimekuwa madhubuti toka kilipoanzishwa kikitoa program tofauti kwa wafanyakazi katika ngazi zote katika benki yetu”, alisema.


Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Benki hiyo, Dinesh Arora alisema kuwa wana sera madhubuti katika kupandisha vyeo na uajiri ambapo nafasi zote za uongozi wa juu wa benki katika matawi yote zimekaliwa na wafanyakazi waliotoka ngazi za chini za uongozi kama Maafisa wa Benki, Wasaidizi wa Wakuu wa Matawi, Mameneja Uendeshaji na kukua mpaka kufikia Mameneja Wakuu wa Matawi.


Alifafanua kuwa sera kama hiyo inahitaji kupewa mkazo kwa kuendeleza wafanyakazi katika ujuzi wa kiuongozi wakati huo huo wakiendelea kutilia mkazo katika kukuza ubora wa ufanyajikazi.Pia alisema kwamba soko la hivi sasa katika sekta ya kibenki lenye changamoto na mazingira ya kiushindani limeshababisha benki hiyo kuona ulazima wa kuwa na mafunzo ili watu waweza kupata elimu, ujuzi na namna bora ya kukabiliana na changamoto zozote katika kazi zao.


Kwa upande wake, Meneja Mafunzo na Maendeleo wa benki hiyo, Priti Punatar alisema kuwa programu ya eMpower iliandaliwa katika kutoa mafunzo tofauti ya ndani katika nyanja za uongozi ambapo kwa sasa zaidi ya wafanyakzio 100 watapatiwa mafunzo husika kwa nyakati tofauti.


 “Program hii itaendelea kwa kipindi cha miaka miwili ijayo kwa kuwa na program bora zaidi ikiwa na lengo kuendelea kukuza ubora katika menejimenti na uongozi na wakati huo huo benki ikiendelea kupandisha madaraja wafanyakazi wake kila mwaka.


Pamoja na wafanya kazi hao pia programu hiyo itatolewa kwa wafanyakazi muhimu ambao hawapo kwenye ngazi za uongozi”, alisema Punatar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...