Intelijensia wa Globu ya Jamii wanathibitisha kwamba Chaka Khan, mwimbaji mkongwe wa muziki wa soul kutoka Marekani, ambaye pia ni maarufu kwa kuwa na miguu mizuri, ametia timu Dar na hivi tunavyobofya ndio ana check-in katika hoteli moja katikati ya jiji la Dar (jina kapuni kwa sasa sababu za kiintelijensia) akiwa na kundi lake la watu kadhaa.

Nusanusa ya maintelijensia wetu zimebaini kwamba Chaka Khana kaja kufanya shoo moja na tukithibitisha jina la waandaaji, tutawafahamisheni. Ila habari za kiintelejensia ndio hizo.
-----------------------------------------------
ON AIR NOW:
Tunaongea laivu na kijana wetu
wa intelijensia  aliye eneo la tukio:

Mkuu: Halloooo, vipi huko?
Kijana: Huku safi tu bosi, Sh'kaooo..
Mkuu: Enhe, huyo Chaka Khan kaja kweli ama umefananisha?
Kijana: Kweli mkuu. Kaja Kweli. Tumetoka nae wenyewe eapoti hadi Hilton hotel
Mkuu: Hilton? Dar pana Hilton kwani??
Kijana: Ipo si ile Double Tree kule nanihiiii.... Dah! wapi vile. Ehh! Nanii....Slipway
Mkuu: Kaletwa na nani na kaja kufanya nini na lini?
Kijana: Mmeletewa nyie na kaletwa na Ubalozi wa Marekani, atapiga shoo Ubungo Plaza Jumamosi hii, kiingilio buku salasini. Yaani mziki na lanchi ya usiku...
Mkuu: Ubalozi wanafanya festivo siku hizi?
Kijana: Ndio. I mean, hapana. Kila mwaka ubalozi huleta burudani toka Marekani. Safari hii mmeletewa nyie vijana wa zamani mkumbuke enzi zenu za boogie YMCA na Mbowe na Motel Agip kwa DJ Emperor.
Mkuu:Una uhakika sio Clouds waliomleta kwa ajili ya Fiesta?
Kijana: Haki ya nani tena bosi. Ni Ubalozi. Wao Clouds ni waratibu tu. Ila wao kwa Fiesta wanamleta Rudikrauzi...sijui...
Mkuu. Sio Rudikrauzi - ni Ludacris
Kijana: Sawa Mkuu. Kuna jingine
Mkuu: Lipo - Picha vipi?
Kijana: Ayaaaah wee...! Nimeacha kamera msalani eapoti (click)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    DUH ENZI HIZO BRAZAMENI ANKAL MICHUZI NDIO NYIMBO HIZI MIE NYIMBO KAMA HII MARA YA MWISHO KUZISIKIA NI RUNGWE BEACH DISCO TOTO... MSHAPAKIWA KWENYE PICK UP AU MNAENDA BAHARI BEACH. KD.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2011

    CLASSIC!! HAHAHAHA RUDIKARAUZI KWELI MUHAYA NI MUHAYA TU HAHAHAHHAAH MBAVU SINA SAFI SANA NIMEIPENDA HII. KK

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2011

    Mmabo ya msimu wa Fiesta nini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...