• Wachezaji wa Red Sea wakiwazonga waamuzi wakilalama kuwa wanaonewa baada ya penati mbili za  Yanga kurudiwa baada ya kugonga mwamba wakati wa mchezo wao wa robo fainali  wiki iliyopita

Na Globu ya Jamii Ripota
Wachezaji 13 kati ya 26 wa timu ya kandanda ya Red Sea ya  Eritrea  waliosepa baada ya kushiriki kombe la Kagame Castle Cup wamejisalimisha katika Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es salaam na kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Msemaji wa Wizara Bw. Isaac Nantanga kaeleza sasa hivi kwamba hivi sasa wachezaji hao wanafanyiwa mahojiano na Idara ya Wakimbizi wizarani humo  kabla uamuzi wa nini cha kuwafanya haujatolewa.

"Mahojiano haya ya awali yanafanywa ili kujua sababu zilizowafanya wachezaji hao kutorejea kwao na kama sababu hizo zinaweza kuwapa sifa ya kupewa hadhi ya ukimbizi kufuatana na sheria za kitaifa na kimataifa.

"Wakati wakiwa hapa nchini wechezaji hao wanahifadhiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na hati zao za kusafiria zinashikiliwa na Idara ya Uhamiaji",  alisema Bw. Nantanga.

Wachezaji hao waliingia mitini juzi wakati timu yao ilipokuwa inataka kuondoka kuelekea nyumbani juzi, baada ya kutolewa na Yanga katika robo fainali. 

TFF waligundua kwamba jamaa wamesepa baada ya kujikuta wana hati za kusafiria 13 wakati msafara wa kwenya uwanja wa ndege ulipoanza. Ndipo wakatoa taarifa kunakohusika na msako ukaanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. ZeroBrainJuly 12, 2011

    Kaka,

    Mi naona wawaonee huruma tu wawaachie wakae nchini kwani wakirudishwa kwao wanaweza kuuwawa hao kwa kisingizio cha kwamba wameiaibisha nchi yao.

    Wawaonee huruma wawaache tu jamani!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2011

    Kazi kwelikweli!! Eritrea hakukaliki jamani,takribani nusu ya watu wa nchi hii wapo nje ya nchi yao.Idadi yao ni takribani 5 mil. lakini 2.5 inasemekana wapo nje ya nchi. Hakuna anayepata nafasi ya kutoka nje ya nchi akapata hamu ya kurudi nchini kwake.Nipo mashariki ya mbali na jamaa tunasoma nao hawatamani kurudi na wanafanya mipango ya kutimkia nchi za watu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2011

    Kwani Eritrea kuna vita sasa hivi? Si ilishaisha?

    Lakini hapo ndio tukubali kuwa Tz ni nchi nzuri japo wengine wanaibeza na kutamani wangezaliwa mbwa ulaya.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2011

    Nimeamini Bongo tambarareeee!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2011

    Hao wanatafuta gea ya kuendea Australia. Tunawajua sana hao, karibia wote wamekimbilia huko halafu wanadharau waafrika wenzao hasa sisi weusi. Wao wanajifanya eti ni kizazi cha wazungu. Mimi siwafagilii kabisa kukaa nchini kwetu. Bora hao UNHCR wawapeleke tu hukohuko Australia wanakokutaka.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2011

    Itumike Busara hapo.Waonewe huruma lakini kwa kufuata Taratibu za Kitaifa na kimataifa.Halafu wanagonga mpira hao watoto ni noma.Wapewe uraia Fasta na waingizwe timu ya Taifa.Wafaransa na nchi zingine wanafanya hivyo..Ni vile!

    David V

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2011

    jamani tubaki bongo mambo ni tambarare! si mnaona watu wanazamia wakati nyinyi mnataka kukimbia!
    TZ tuko juu!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2011

    oh hao ndio kawaida yao.huwa wanafanya hivyo kila nchi wanayokwenda.Mpaka dakika hii wanaitwa (Political immigrants) wana akili sana.hata kama serikali ya bongo haitawachukua watapelekwa USA, Australia,Canada na kwingineko wakaishi kama political immigrant. na wakapige box. Akili ku mkichwa ndugu yangu.kaa hapo unashangaa mawe.
    Immigration najua ni watu wazuri watawapa ushirikiano.
    Mdau mwana maendeleo na mchambuzi wa uchumi wa kisiasa(Political economy)kusoma raha jamani!!!! Asante Mungu.
    Diana ROK.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2011

    hapana mimi sikubaliani kabisa na watu wanaosema waonewe huruma waruhusiwe kubaki nchini...warudishwe kwao tena chini ya usimamizi mkali wakibaki hao ndio wanaoletaga vurugu na kuuwa watu sio watu wanaokuwa na utu ni wachache sana ndio huwa wanakuwa na utu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2011

    wana jamii tusipate mshangao au kuona jambo hilo ni geni maana hiyo tabia inaongozwa na sisi watanzania kwenye safari zetu za michezo mbali mbali kama olimpic huwa tunafika ulaya tukiwa wengi na hupata safari hizo kwajili ya michezo na tukifika huko wengi wetu hukimbia na kuingia nchi tofauti za ulaya kuomba ukimbizi na baadae kubeba boks

    mbeba boks mkimbizi kama hao wa eritrea.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 12, 2011

    wabongo wanawaza kwenda ulaya kujilipua hapa waeritria wanazamia tz. kazi ipo

    ReplyDelete
  12. nshimimana aka dumisaneJuly 12, 2011

    i love you bongo, japo sijafika

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 12, 2011

    Tanzania watakaa kwa muda tu,wako safarini to South Africa hao.Wasaidieni hali ya Eritrea na Ethiopia ni mbaya sana kwa vijana, nilishawai kupita huko kikazi.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 12, 2011

    We Diana umewaona wapi tena wakiomba hifadhi? Wabongo Bwana, wachunguzeni kwanza kama hawana mabomu maana hiki kizazi cha Obama huwa hawaaminiki. Pia kama nchi inaweza kuwasaidia iwasaidie ila sheria ifuate mkombo maana shortcut Tz ni nyingi na hawa jamaa wanaweza liletea Taifa balaa. But is good to show them charity heart but tell them that even our vijanas they are strugling to feed themselves because our Serikalis they don't have enough peses to help them but they just show love for foreigners not for citizen. Is not like Ulayas ukiwa jobless unalipwa. Na pia wasiwapende watoto wetu wa kike please.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 13, 2011

    Kuna njaa ya kufa mtu kutokana na ukame, angalieni world news, hebu waacheni hao kaka zangu wabaki hapo TZ hata kama wataondoka kwenda US au Australia au South Afrika wewe unayesema warudishwe kwao watakupunguzia nini? Hata wakibaki utapungukiwa na nini? Mnakuwa kama wazungu kutwa kulialia na immigrants wakati wao wavuvi kufanya kazi za hovyo hovyo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 13, 2011

    watu wako "ON TRANSIT", [HAO WANAPITA TUU] hao hawataki bongo wala nini washapunguza gharama za usafiri na malazi na hawajaingia Tz kinyume cha sheria. WAKENYA WENYEWE BONGO NI "DEAL" KWAO, WANAOA/OLEWA MTAANI "LEFT N' RIGHT" ...

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 13, 2011

    Mnajifanya mna huruma. Nyoooo! hao jamaa hawafai kabisa kupewa uraia. Ni wa kupelekwa hukohuko Canada na Australia wanakokutaka. Hapo bongo wanapatumia tu kama njia ya kupita. Twawajua hao hawataki kukaa kwao. Sasa hivi wenzetu toka Afrika magharibi, kaskazini na kaskazini mashariki mkakati wao ni kutimkia nchi zingine zilizoendelea kwa kutumia visingizio vya aina yoyote ile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...