Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa David Msuya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernand Membe wakiwa na waomolezaji wengine katika kuaga miili wa Marehemu Sekou Toure Mndeme, aliyekuwa Mkurugenzi wa CRDB tawi la Lumumba aliyefariki huko India Julai 13, 2011, pamoja na mtoto wa baba yake mdogo marehemu Sheni Sultani ambaye naye  alifariki Julai 10, 2011 katika hospitali ya Amana jijini Dar. Shughuli hii imefanyika leo nyumbani kwa hayati Sekou Toure Kunduchi Mtongani, jijini Dar, kabla ya miili ya marehemu hao wawili kusafirishwa kuelekea Usangi kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa
 Waombolezaji wakijiandaa kuombea miili ya marehemu Sekou Toure Mndeme na Sheni Sultani leo
 Miili ya marehemu ikitolewa nje ili kuswaliwa, kuangwa na hatimaye kusafirishwa

 Mwakilishi wa benki ya CRDB akitoa rambirambi za mahali alikokuwa akifanyia kazi Sekou Toure
 Sehemu ya waombolezaji
 Ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu
 Waombolezaji msibani
 Mwili wa Sekou Toure ukiwasili nyumbani kwake
 Mwili wa Sheni Sultani ukiwasili
 Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa David Msuya akisaini kitabu cha maombolezi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisaini kitabu cha maombolezo. Karibu naye ni kaimu mkuu wa mkowa wa Dar es salaam Mhe. Mecky Sadiki
Sahihi katika kitabu cha maombolezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...