Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Klabu mpya ya michezo inayojulikana kama “Biafra Jogging and Sports Club” inatarajiwa kuzinduliwa Jumapili tarehe 24 Julai mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa kamati ya bonanza la uzinduzi huo Abdul Mollel amesema uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya Biafra Kinondoni Dar es Salaam kuanzia saa moja na nusu asubuhi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Diwani wa kata ya Kinondoni Bi. Husna Hemed.

Uzinduzi huo utaambatana na kukimbia (jogging) umbali wa kilomita kumi (10) kuanzia kinondoni B kuelekea Mwananyamala mpaka viwanja vya Biafra.

Mollel amesema madhumuni ya klabu hiyo ni kuiweka jamii pamoja ili kushiriki katika mazoezi ya viungo na michezo kwa ujumla ikiwa ni njia ya kujiimarisha kiafya na kujiepusha na vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya mtanzania.

“kwa kupitia klabu yetu hii mpya ya michezo tutajitahidi kuwahamasisha wananchi kushiriki katika michezo ili kuepukana matatizo mbalimbali kama utumiaji wa madawa ya kulevya, ukahaba, ulevi wa pombe kupindukia, uzururaji pamoja na vitendo vinavyochangia kueneza ugonjwa wa UKIMWI,” amefafanua Mollel.

Mollel ameongeza kuwa clubu hiyo itaendelea kujihusiaha na shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo kutembelea na kusaidi watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na utunzaji wa mazingira.

Mbali na kukimbia kutakuwa na michezo mingine itakayofanyika katika uzinduzi huo. Michezo hiyo ni mpira wa miguu, kukimbiza kuku, mpira wa kikapu pamoja na kuvuta kamba.

Aidha wakati wa mchana mara baada ya kukamilika kwa shughuli za michezo kutakuwa na burudani ya muziki kutoka bendi ya mapacha watatu, bendi ya shengena na vijana kiduku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...